Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
(UNWTO), Zurab Pololikashvili amesema moja ya kipaumbele chake kwa sasa
ni kuhakikisha Afrika inafanya vizuri katika masuala ya utalii ili kuongeza
ajira kwa wananachi wenye nia ya kutaka kujihusisha na shughuli ho
ya Utalii
📌MWANDISHI WETU, CAPE VERDE.
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii (UNWTO)
limeichagua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Utalii
wa 65 wa Kanda ya Afrika utakaofanyika Jiji la Arusha Oktoba,2022.
Mkutano huo, utajumuisha Mawaziri wote wa Utalii wa Bara la Afrika huku ukitarajia
kuongeza tija kwa Tanzania kwenye fursa za kukuza Utalii Kimataifa.
Akizungumza jana nchini hapa katika kisiwa cha SAL, Cape Verde,
katika mkutano huo wa siku Nne mbele ya zaidi ya Mawaziri 30
wa utalii, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro
amewashukuru Mawaziri hao kwa kuipa heshima nchi ya Tanzania huku akiowaomba
mawaziri wote wa utalii kuja kushiriki katika mkutano huo mwakani.
Katika uchaguzi huo uliowakutanisha mawaziri 30 wa utalii wa Bara la
Afrika, Mawaziri hao waliridhia kwa kauli moja kuwa Tanzania ina sifa
zote za kuwa mwenyeji wa mkutano huo mara baada ya Tanzania kuwa nchi pekee
iliyokuwa imeonesha nia ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Kufuatia hali hiyo Tanzania inakuwa ni nchi ya kwanza kupita bila kupingwa na
katika mkutano wa Kimataifa wa utalii wa 64.
Akizungumzia manufaa ya mkutano huo, Dkt. Ndumbaro
amesema kufanyika mkutano huo nchini utaiweka Tanzania katika
ramani ya dunia kwa kutangaza fursa uwekezaji katika sekta ya utalii pamoja na
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Waziri wa Utalii wa Gambia, Hamat Bah mara bada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutanao huo
Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema kitendo cha Mawaziri wote kuridhia
kwa kauli moja kuwa Tanzania iwe mwenyeji wa mkutano huo ni imani kubwa
ya waliyonayo kwa nchi ya Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla
Dkt. Ndumbaro amesema kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ni hatua
mahsusi kwa nchi kujitangaza kimataifa kwa vile washiriki mbalimbali
duniani watahudhuria mkutano huo wakiwemo wabobezi wa utalii pamoja
na makampuni makubwa ya kutangaza vivutio vya utalii kutoka nje
yatatangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na Afrika kwa ujumla
Kwa upande wake Waziri wa Utalii na Mambokale wa Zanzibar, Mhe. Lela Mohamed
Mussa amesema utachagiza idadi ya watalii watakaoitembelea Tanzania kupitia
mkutano huo.
Tunajisikia fahari kuona ajenda yetu kama nchi ya kuja kushiriki katika mkutano huu umefanikiwa na tuna matumaini makubwa kuwa mkutano huo utatangaza vivutio vya utalii vilivyoko Zanzibar na Tanzania bara
. Lela Mussa.
Aidha, Katika mkutano huo Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Bajeti na Mipango ya UNWTO kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu kuanzia sasa Naye Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvili amesema katika kipindi chake cha uongozi moja ya kipaumbele chake kikubwa ni kufanya uwekezaji katika bara la Afrika ili kuongeza ajira kupitia sekta ya utalii.
Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano huo unaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ambaye ameambatana na Waziri wa Utalii na Mambokale wa Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa
Pia Wajumbe wengine walioambatana na Mhe. Waziri ni pamoja Kamishna
Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, Kamishna Uhifadhi kutoka TAWA, Mabula
Misungwi, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga , Balozi wa
Tanzania Paris, Mhe. Samweli Shelukindo pamoja na maofisa kutoka Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) , TTB pamoja na TANAPA
Rais wa Cape Verde, Dkt. Jorge Carlos Fonseca akiwa kenye picha ya pamoja na Mawaziri wa Utalii Barani Afrika mara baada ya kufungua mkutano wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, wa tatu kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro.
0 Comments