📌DOTTO KWILASA
SERIKALI imedhamiria kuimarisha kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu na kuwa cha kibiashara Kwa kuondoa uhaba
wa maafisa ugani ambao unaikabili sekta hiyo.
Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wakati akifungua mafunzo rejea ya kanuni bora za zao la Alizeti kwa maafisa ugani wa Tarafa na Kata toka katika Mikoa ya Singida,Dodoma na Manyara .
Aidha mafunzo hayo yana lengo la Kuongeza uzalishaji wa alizeti na mkakati wakuongeza kipato cha maafisa ugani katika mikoa yote nchini na nguvu kubwa itaongezwa katika mikoa inayolima kwa wingi zao la alizeti.
Akiongea kwenye uzinduzi huo amesema kwa Sasa
kuna uhaba wa Maafisa hao ambapo Kwa sasa idadi yao ni 6704 sawa na
33% huku mahitaji ya maafisa hao ikiwa ni 20,538.
Ili kuinua kilimo tunatarajia kuboresha miundombinu ili kuzalisha mazao kwa wingi na kukidhi mahitaji ya viwanda vya ndani na ziada kuuzwa nje ya nchi.
Profesa Mkenda amesema hali hiyo
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji wa zao la mkakati la alizeti na
kuondokana na Uhaba wa mafuta ya kupikia ambao hutokea mara kwa mara.
"Hapo awali Kilimo cha alizeti nchini
hakikupewa kipaumbele hali ambayo ilipelekea zao la alizeti kutokuwa na
tija na hivyo uzalishaji kushuka huku akiwataka maafisa ugani nchini
kuwa na mashamba darasa ya alizeti pamoja na mashamba yao wenyewe ili yawe ya
mfano ikiwa n pamoja na kujiongezea kipato,"amesema.
Ameongeza kuwa ,maofisa ugani walikuwa
hawatumiwi ipasavyo katika kilimo na kutaka shughuli za kilimo kuangaliwa upya
ili kilimo kiweze kuwa cha tija ambapo Serikali itashirikiana na Tamisemi
katika kuwawezesha maofisa ugani ili kuwafikia wakulima na kuzalisha
ajira kwa vijana wahitimu kupitia kilimo .
Kwa Mwaka wa Kilimo 2021/2022 tutahakikisha changamoto za mbegu na pembejeo za kilimo zinapatiwa ufumbuzi ili suala la kilimo liweze kufanikiwa ipasavyo pamoja na kutatua changamoto ya uhaba ya maafisa ugani.
Awali akitoa taarifa kuhusiana na mafunzo hayo,Mkurugenzi wa mafunzo,huduma za ugani na utafiti toka Wizara ya Kilimo,Dk Wilherm Mafuru kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo amesema kuwa mafunzo rejea ya kanuni bora ya zao la alizeti toka mikoa ya singida,Dodoma na manyara ambayo ndio mikoa kielelezo katika kukuza zao la alizeti huku lengo ni kufanya mafunzo kwa mazao yote.
0 Comments