📌AMANI KASSIMBA
WAKALA
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) imefanikiwa kununua tani 4,600 za
mahindi zenye thamani ya Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia tatu (
2,300,000,000) toka kwa wakulima kati ya lengo la tani 5,000 zilizopangwa awamu
ya kwanza kufikia Agosti 31, mwaka huu.
Hayo
yamebainishwa leo (01.09.2021) wakati Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Joseph Mkirikiti ofisini kwake Sumbawanga akiwa katika ziara ya kukagua zoezi
la ununuzi wa mahindi Meupe linaloendelea katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Lupa
aliongeza kusema serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuendelea
kununua mahindi ya wakulima kulingana na upatikanaji wa fedha.
Wakala unaendelea kufuatilia fedha toka Serikalini ili itekeleze jukumu la kununua mahindi ya wakulima kama ilivyopangwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 hivyo wananchi wa Rukwa wawe na subira
Lupa
aliongeza kusema Wakala unaendelea kukamilisha ujenzi wa vihenge vya kisasa na
kuwa lengo mahindi yote yatakayonunuliwa Rukwa msimu huu yahifadhiwe .
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti alisema wananchi wa Rukwa
wamezalisha kwa wingi mahindi kwa kuwa ni zao lao la biashara hivyo wanategemea
zaidi NFRA kama soko la uhahika.
Tunaendelea kuiomba serikali itupatie mgao zaidi sisi wana Rukwa kwani zao letu la mahindi ndio zao la biashara kwa wananchi wengi
Kwa
mujibu wa takwimu za uzalishaji wa mazao ya chakula kilimo msimu wa 2020/2021
mkoa wa Rukwa ulizalisha tani 651,433 za mahindi kati ya lengo la tani 731,500
ambapo kutokana na uzalishaji mkubwa mkoa una ziada ya mahindi tani 354,117.
0 Comments