📌DOTTO KWILASA
WAZIRI wa Maji nchini
Juma Aweso amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan ameidhinisha kiasi cha shilingi Bilioni 207 kwa ajili ya kurahisisha
upatikanaji wa maji Vijijini ikiwa ni dhamira yake ya kumtua Mama ndoo kichwani.
Mbali na fedha hizo Bunge la Bajeti pia liliidhinisha bilioni 680 kwa Wizara hiyo ili kwenda kutekeleza miradi ya maji mijini na vijijini na kutatua kero ya maji.
Aweso ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye mkutano wake na vyombo vya Habari nchini uliolenga kutoa shukurani kwa vyombo hivyo kwa namna ya pekee ambavyo vimetoa ushirikiano kwenye Wizara hiyo na kupelekea kupatikana kwa mafanikio mbalimbali.
Hatua hii imekuja huku
Wizara hiyo ikiwa katika mkakati wa kuhakikisha inafikia asilimia 95 ya
upatikanaji wa maji mijini huku ikipata fedha Zaidi ya dola milioni 500 ambazo
ni sawa na zaidi ya shilingi Tirion moja iliyotokana na mahusisano mazuri
kati ya Tanzania na Serikali ya India kupitia Exim Bank.
Waziri huyo wa Maji
ameeleza kuwa fedha hizo zimeelekezwa kwenye miradi ya Maji katika miji 28 na
kwamba vibali tayari vimepatikana na utekelezaji wake utaanza hivi karibuni
hali itakayosaidia wananchi kupata huduma ya maji safi na salama.
Mojawapo ya Miji hiyo ni Makambako,Wanying’ombe,Muheza,Handeni na maeneo mengine ili kuhakikisha tunatatua matatizo ya maji ya watanzania mijini na vijijini
Licha ya hayo ameeleza
kuwa katika maeneo ya Vijijini kupitia fedha zilizoidhinishwa na Bunge pamoja
na zilizoongezwa na Rais Samia ,Wizara kwa kushirikiana na wakala wa maji
vijijini (RUWASA)itaendelea kutoa maelekezo mahsusi kwa wahandisi wote wa maji
kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata maelekeo ya wizara hiyo ili kutatua kero ya
maji.
Pamoja na mambo
mengine,ameeleza kuwa ili kuhakikisha Wizara hiyo inafanikiwa kuingia asilimi
85 ya upatikanaji wa maji Vijijini ,kwa mwaka huu imepanga kuingia mikataba
1176 kwa ajili ya kuhakikisha wanajenga miradi ya maji vijijini kwa kuzingatia
kuwatumia wakandarasi wenye uwezo.
“Tumezingatia
Wakandarasi wasio na uwezo hawatapata miradi,wakandarasi wazuri wanafahamika na
wakwamishaji wanafahamika,moja ya changamoto ya ukwamishaji wa miradi ya maji
ni wakandarasi wababaishaji wasio na uwezo hatuwezi kuwapa nafasi kwenye wizara
yetu,”ameeleza.
Pia Aweso amewataka
Wakandarasi wataoingia mkataba na wizara hiyo kulichukulia suala la maji kama
vita mahususi ya kuhakikisha watanzania waishio vijijini wanaondokana na kero
ya maji na kuwa na uhakika wa kupata maji wakati wote.
Si busara hata kidogo kuona leo mradi wa maji unakwamishwa kwa kukosa fedha kwa ajili ya ubadhilifu,tunataka wananchi wapate manufaa kutokana na serikali yao hakuna usiri wowote kwenye miradi hii ya maji,tunataka kila kitu kiwe wazi
Katika hatua nyingine
,Waziri huyo mwenye dhamana ya usimamizi wa maji nchini amezungumzia hali ya
upatikanaji wa Maji kwa Jiji la Dodoma ambapo ameeleza kuwa bado kuna uhitaji
mkubwa wa maji ambapo uwezo wa uzalishaji wa maji kwa sasa ni lita milioni 66
huku mahitaji yakiwa ni lita 103 kutokana na ongezeko la watu.
Kutokana na hayo Aweso
ameeleza kuwa zipo jitihada ambazo wizara hiyo imefanya kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma(DUWASA) kwa kuchimba
visima maeneo ya pembezoni na kuongeza tenki kubwa eneo la Buigiri ili
kuhakikisha maeneo ya Soko la Ndugai,Nzuguni,Njedengwa yanapata maji ifikapo
mwezi wa kumi mwaka huu.
Akieleza kuhusu azma
ya mkutano wake na Waandishi wa Habari,Waziri Aweso ameeleza kuwa bila vyombo
vya Habari wizara yake isingefanikiwa .
Amefafanua kuwa
kupitia vyombo vya Habari wananchi wamekuwa wakipa taarifa mbalimbali
zinazohusu utekelezaji wa maji na kuwafanya kuendele kuzitatua changamoto
ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph amewatoa wasiwasi wakazi wa Jiji la Dodoma kuwa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya maji itahakikisha inatatua kero zote za maji kwa kufanikisha miradi yote ambayo inaendelea kutekelezwa.
0 Comments