📌LUCY NDALAMA
MKUU wa Mkoa wa
Dodoma,Anthony Mtaka ameitaka Benki ya Biashara Tanzania (TCB)
kuwaonesha wanawake na kuzifuata fursa ambazo zipo katika maeneo
mbalimbali na kisha kutoa fedha kwa wajasiamali wanawake ili
waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza leo
Septemba 8,2021 wakati wa uzinduzi wa kongamano la wanawake na biashara ambalo
liliandaliwa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka Benki
hiyo kuzifuata fursa mbalimbali na kisha kutoa fedha kwa wanawake ili waweze
kujiongezea kipato kupitia fursa hizo.
Katika kongamano hilo
wanawake wajasiriamali walipata fursa ya kuifahamu TCB ambapo pia
ziliwasilishwa mada mbalimbali ikiwemo nafasi ya mwanamke katika kukuza uchumi
wa Taifa,ambapo jumla ya washiriki 350 hasa wanawake walishiriki
Hapa nitawaleta watu wanaojenga Standard Gauge,Tarura na wale wa Bomba la Mafuta waje waseme fursa kwao zipo katika maeneo yapi halafu nyinyi muwape fedha wanawake ili ikiwezekana wasambaze vyakula katika miradi hii
Aidha,amesema
changamoto kubwa kwa wanawake ni kukopa mikopo umiza lengo likiwa ni
kufanikisha ndoto zao ambapo amedai jambo hilo limekuwa likiwarudisha nyuma
hivyo Benki hiyo inatakiwa iwasaidie wapate mikopo yenye riba nafuu.
"Mkurugenzi Mtendaji tafuta
‘position’ ukijikita kwa wanawake benki yako itakuwa kubwa,hawa wanawake
unaowaona hapa wanakopa shilingio 500,000 marejesho shilingi milioni 2 au
nakosea(wanashangilia) wasaidieni hawa wajasiriamali kutoka kwenye mikopo
umiza,”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Pia,amesema jukwaa la
wanawake na biashara linaendana na mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa
kuongeza ushiriki wa wanawake katika kushiriki na kusimamia uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake,Afisa
Mtendaji Mkuu wa TCB,Sabasaba Moshingi amesema atashirikiana na Mkuu wa Mkoa
kuhakikisha wazifuata fursa hizo ikiwemo kwenda katika baadhi ya Mikoa.
Hata hivyo, amesema
benki hiyo inawajibu kuupa kipaumbele uwekezaji wa wanawake na maendeleo yao
baada ya Serikali kuziunganisha shughuli zake na zile za iliyokuwa Benki ya
wanawake Tanzania.
Amesema lengo la
kongamano hilo ni kuwakusanya wanawake ili waweze kujadiliana kwa pamoja jinsi
ya kukuza biashara zao na kuweza kufanikiwa katika maisha yao hivyo kuikwamua
jamii kiuchumi.
Aidha,amesema kwa sasa
zipo huduma maalum zinazowalenga kina mama kama akaunti ya Tabasamu na dirisha
maalum kwa ajili yao kwenye matawi ya benki na huduma za bima maisha
kwa vikundi ambavyo wanachama wake wengi ni wanawake.
Naye,Mbunge wa Viti
Maalum,Fatma Toufiq amewataka wanawake nchini kupendana kuheshimiana pamoja na
kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza huku akiiomba
Serikali kuendelea kuwapa kipaumbele katika mambo mbalimbali.
0 Comments