📌MWANDISHI WETU
KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi Anna Makinda
amewaasa wananchi wa Kata ya Dodoma Makulu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma
kujitokeza kwa wingi siku ya kufanya sensa ya majaribio ya watu na makazi
ambayo inayotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 11 hadi 13, 2021 katika Kata
hiyo ikiwa ni majaribio ya kupima nyenzo zilizoandaliwa ikiwemo mifumo ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) itakayotumika katika zoezi hilo
nchi nzima mwakani.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na
wananchi wa Kata hiyo uliofanyika katika uwanja wa Ofisi ya Mtendaji wa Kata na
kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri, Diwani wa Kata hiyo
Fadhili Chibago pamoja na Wenyeviti wa Mitaa
Najua watu wa umri wangu sense sio jambo geni,mpaka sasa tunasemasema tu sijui tupo million 60 hakuna anayejua ukweli,hivyo kupitia sense tutajua ukweli kuhusu idadi ya watu waliopo nchini.
Akiwaeasa wakazi hao kutoa ushirikiano mkubwa kwa mawakala wa sensa ya majaribio na wale watakaofanya sensa rasmi mwaka 2022, Makinda aliwaomba wananchi hao kutoa taarifa sahihi kwa kila swali litakalo ulizwa pasipo kuwa na udanganyifu wowote ili Serikali ipate taarifa sahihi kuhusu watu na makazi, lakini pia sensa ni siri na mawakala hao wameapa kutunza siri.
Akizungumzia lengo la zoezi la sensa ya majaribio
ya watu na makazi, Kamisaa Makinda alisema ni kupima utayari wa watendaji na
maandalizi ya watendaji wa sense katika kuhakisha kila kitu kinakwenda sawa
mnamo mwaka 2022.
Alisema idadi ya mikoa iliyotengwa kwa ajili ya
sensa ya watu na makazi ya majaribio ni 18, ikiwemo mitano ya Zanzibar na kwa
Tanzania Bara ni Mikoa 13 ikiwemo mkoa wa Dodoma ambapo kata hiyo ya Makulu
itatumika kwa majaribio.
Awali
wakati akimkaribisha Kamisaa Makinda, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri
alisisitiza kuwa, sensa ya watu na makazi ni muhimu na kila mwananchi ni haki
yake kuhesabiwa ili kutambulika na serikali.
Sensa ya watu na makazi itafanyika rasmi mwaka
2022 ikiwa ni sensa ya sita tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na hufanyika
kila baada ya miaka kumi.
0 Comments