📌NTEGHENJWA HOSSEAH (TAMISEMI)
WANAFUNZI Takribani 1,132,143 waliosajiliwa kutoka
katika shule za Msingi 17,585 za Tanzania Bara wameanza mitihani yao ya
kuhitimu elimu ya msingi. Kati ya hao wavulana ni 547,502 sawa na asilimia
48.36 na wasichana ni 584,641 sawa na asilimia 51.64
Kati ya Watahiniwa 1,132,143 waliosajiliwa
watahiniwa 1,079,943 sawa na asilimia 95.39 wanafanya mtihani kwa lugha ya
Kiswahili na watahiniwa 52,200 sawa na asilimia 4.61 wanafanya mtihani kwa
lugha ya Kingereza.
Aidha watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 3,327, kati yao 108 ni wasioona, 951
wenye uoni hafifu,739 wenye uziwi, 358 ni wenye ulemavu wa akili na 1,171 ni
wenye ulemavu wa viungo vya mwilini.
Kwa mwaka 2020 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 1,023,950 hivyo kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 108,193 sawa na asilimia 10.57 kwa mwaka 2021 ukilinganisha na mwaka 2020
Mitihani hii inalenga kuwapima uwezo na uelewa wananfunzi katika yale yote waliyojifunza kwa kipindi cha miaka saba.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la
Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde.
0 Comments