📌ZAINABU MTOI NA JOSEPHINE MTWEVE
MRATIBU wa Mfuko
wa Bima ya Afya wa Jamii wa jiji la Dodoma, Patrick Sebigya ametoa wito kwa
wafanyabiashara wadogo kujiandikisha kupata huduma ya bima ya afya ili
kuhakikisha usalama wa afya zao.
Akizungumza katika
banda la wakala wa uelimishaji na uhamasishaji wafanya biashara wa soko la
majengo leo jijini Dodoma, Sebigya amesema wameona ni vema kusogeza huduma ya
bima karibu na wafanyabiashara wa eneo hilo kusogeza huduma hiyo karibu yao.
Amesema hawawezi kufanya shughuli zao za kiuchumi
ikiwa afya zao zinayumba ila wakishakuwa na bima ya afya wanakuwa na uhakika wa
afya zao.
‘’Lengo kubwa ni
kuhakikisha kila mwananchi anapata kadi ya bima ili tufikie asilimia 30 ya kaya
zilizopo ndani ya jiji la Dodoma,’’ amesema.
Sebigya amesema
kwa kutumia njia ya Wakala katika maeneo ya masoko watawafikia watu wengi zaidi katika jiji la
Dodoma
‘’Wito wangu kwa wafanyabiashara waliopo hapa
waone hii ni fursa ya dhahabu kwamba wasogee hapa waweze kupata huduma za
matibabu na awe na amani moyoni,’’ amesema.
Aidha wakala wa
uandikishaji wa Shirika la Mfuko wa Bima ya Afya kwa Jamii, Kelvin Sogoe
amesema wanakutana na changamoto nyingi kwasababu baadhi ya watanzania wana mawazo potofu kuhusu uwepo wa wakala
katika meneo yao..
Amesema wakati
wanaweka kituo hicho baadhi ya watu walikimbia eneo hilo wakifikiri kwamba ni kampeni ya serikali
kujaribu kutoa chanjo ya UVIKO-19.
Sogoe amewasihi
wafanyabiashara kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili kujiwekea uhakika wa
matibabu.
‘’Si vema usubiri uanzae kuumwa ndiyo uanze
kutafuta bima ya afya,tunatakiwa kujiandaa mapema kabla hatuja shambuliwa na
magonjwa’’ amesema.
Vile vile mmoja
wa wafanyabiashara wa soko la majengo, Mariam Rugenesi amesema wanaelewa kuwa
bima ni muhimu kwa vile gharama za matibabu kwa sasa zipo juu tofauti na kipato
cha watu wengi wa hali ya chini.
Amesema
anawashauri wafanyabiashara wenzake kukata bima ya afya ilikuepusha gharama za
hospitali pale wanapokuwa hawana bima.
0 Comments