📌DOTTO KWILASA
KUTOKANA na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) Hivi karibuni kudai kuwa kutakuwa na upungufu wa mvua msimu ujao wa kilimo,Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua tani 100,000 za mahindi katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini kuondokana na Uhaba wa chakula.
Hatua hii imekuja wakati ambapo tayari Serikali imekwishanunua tani 24,000 kiasi ambacho kimeelezwa Kuwa ni kidogo na kwamba hakiwezi kukidhi mahitaji ya Wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 6,2021,na Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo wakati akiongea na Waandishi wa habari huku akifafanua kuwa mwezi wa saba Sekretarieti ya Chama hicho ilifanya ziara katika Mikoa ya Rukwa,Songwe na Mbeya ambapo walikutana na changamoto ya wakulima kukosa soko la zao la mahindi.
Amesema mara baada ya ziara hiyo waliiagiza Serikali kununua mahindi hayo ambapo ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 14 ambazo zilinunua zaidi ya tani 24,000.
Amedai kwa
sasa
fedha hizo zimeisha na wakulima wanaendelea kuhangaika kutafuta
soko la kuuzia mahindi yao
Kutokana na hali hiyo
Katibu Mkuu huyo ameiagiza Serikali kutoa tena fedha na inunue tani 100,000 za
wakulima hao kwani wanazotaarifa kwamba msimu ujao wa kilimo mvua zitakuwa
chache.
Pia amesema katika ziara hiyo wamejifunza kwamba uchache wa vituo vya kununulia mahindi hivyo ameiagiza NFRA kuweka vituo ambavyo vitakuwa karibu na wakukulima.
Kuna malalamiko kukatwa fedha katika shilingi 500 tunasema hapana mtu aliyepo Mufindi,Ileje,Mbozi,Nkasi tunataka bei ya mahindi iwe moja kwa wote wa karibu na mbali
Katika hatua
nyingine,Katibu Mkuu huyo ameziagiza Wizara za Kilimo na Fedha na Mipango
wakutane kujadiliana jinsi ya kupunguza bei ya mbolea kutokana na kuwa juu
hivyo kumuumiza mkulima.
0 Comments