📌MWANDISHI WETU
SERIKALI ya
Canada imeahidi kuisaidia Tanzania katika kuimarisha Sekta ya Afya, Elimu na
Mazingira kutokana na ufanisi katika usimamizi wa fedha katika miradi
inayotekelezwa nchini kwa ushirikiano wa Serikali hiyo.
Hayo
yamebainishwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba wakati wa mkutano wake na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Mhe. Pamela
O’Donnell, ulioangazia ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Sekta ambazo Serikali ya Canada imeahidi kuzisaidia zinaumuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi kwa kuwa pia ni sekta za kipaumbele katika Serikali ya Awamu ya Sita.
Alisema kuwa
Tanzania na Canada zitaanzisha mazungumzo mapya ya namna ya kuendeleza programu
za maendeleo zilizokuwa zikifadhiliwa na Serikali ya Canada baada ya progamu
iliyokuwepo kumaliza muda wake mwezi Juni, 2021.
Aidha
alisema kuwa Canada imeisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo
ikiwemo ya Sekta ya madini, elimu, afya na utawala bora yenye thamani ya
takribani dola bilioni 2.39 tangu Tanzania ilipopata uhuru.
Waziri wa Fedha na Mipango amemshukuru Balozi huyo wa Canada kwa kutambua juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi bora unaotambuliwa Duniani kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
Kwa upande
wake Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Mhe. Pamela O’Donnell, alisema kuwa kuna
mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa
nchini Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Canada hususani katika Mfuko wa
Afya na Elimu, ambapo fedha zilizotolewa zimetumika kikamilifu katika masuala
yaliyokusudiwa.
Kutokana na jitihada za Serikali katika kutekeleza miradi, tunaona kuna fursa ya kuendeleza ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya na kuwajengea uwezo wanawake
Mhe. Balozi Pamela O’Donnell.
Picha &Habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -WFM
0 Comments