📌MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Kongwa Remedius Mwema amelipongeza
shirika la World Vision Tanzania kwa
kuwezesha wananchi 1800 kutoka wilaya
hiyo kupata uhakika wa matibabu baada ya
kuwapatia bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kadi za CHF zenye thamani ya 9m/= kwa kaya 300 katika kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa,DC Mwema ameyataka mashirika mengine kuiga mfano wa
World Vision katika kujali afya za wananchi.
Tunazungumzia uchumi,hatuwezi kuwa na uchumi mzuri kama wananchi hawana afya nzuri.Hivyo nawapongeza sana World Vision kwa kujali afya za wananchi kupitia bima ya afya.
DC Mwema pia amewataka viongozi vijiji na kata katika
wilaya hiyo kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko
wa bima ya afya kwani kufanya hivyo kutasaidia uboreshwaji wa huduma za afya
katika maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya pia amewataka viongozi hao kuweka
ajenda ya bima ya afya katika kila kikao wanachokifanya ili iwe sehemu ya
kuhamasisha wananchi ili kufikia asilimia 40 ya kaya zote katika wilaya ya
Kongwa.
World Vision wametuonesha mfano,nawapongeza sana kwa hili.Tuendelee kuhamasisha wananchi katika maeneo yetu ili kaya nyingi zaidi wajiunge kwenye mpango huu wa bima ya afya.
Baadhi ya wanufaika wakipokea kadi zao za CHF kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa |
Naye mganga mkuu wa wilaya ya Kongwa Dkt.Thomas Mchomvu ameshukuru shirika hilo kwa nia yake ya dhati ya kuboresha afya kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Dkt.Thomas amesema awali ambi lililomfikia kutoka
shirika hilo ni kuhudumia watoto lakini baada ya majadiliano na watendaji wa
shirika hilo walikubali kutoa bima kwa familia nzima ya walengwa.
Niwashukuru kwa ‘flexibility yenu,maana tungemuhudumia mwanafunzi tu mambo bado yangekuwa magumu siku mzazi atakapoumwa,bado huyohuyo mwanafunzi angepata mzigo wa kuuguza hivyo walikubali kuiunganisha kaya yote
Pia ameongeza kwamba maelekezo yaliyopo wilaya
Kongwa inatakiwa kufikia 30% kutoka 12% ambayo ni sawa na kaya 7264
zilizojiunga na CHF kati ya kaya 61995 zilizopo wilayani hapao.
Kaimu Mratibu wa Mradi eneo la Kongwa Zacharia Shigukulu akisoma ripoti ya mradi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa |
Baadhi ya wananchi walioudhuria halfa ya kukabidhi kadi za bima ya afya ya CHF |
Kwa upande wake Kaimu mratibu wa mpango huo eneo la
Kongwa,Zacharia Shigukulu amesema kwamba mpango huo unatekelezwa katika awamu
mbili na awamu ya kwanza .
Pia Shigukulu amebainisha kwamba mpango huo
unatekelezwa katika vijiji 10 vilivyopo katika kata ya Makawa,Matongoro pamoja
na Mkoka ikitarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi 36,621 kutoka kwenye kaya
8027.
Kaimu Mratibu pia amesema malengo ya mradi huo ni
kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha afya na ustawi wa watoto na
familia zao na maisha ya jamii na katika kaya hizo 300 zilizokabidhiwa kadi zinajumuisha
watoto 1200 na watu wazima (wazazi/walezi) 600.
Burudani ya ngoma za asili zilikuwepo pia |
0 Comments