📌NTEGENJWA HOSSEA
WAZIRI TAMISEMI Ummy Mwalimu amewakabidhi Mikononi
mwa Polisi viongozi wa Kijiji cha Nyamililo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema
Mkoni Mwanza kwa kuchangisha wananchi michango bila Kibali cha Mkuu wa Wilaya.
Waziri Ummy amechukua hatua hiyo wakati wa ziara
yake Wilayani humo ambapo alitembelea Zahanati ya Nyamililo kukagua maendeleo
ya ujenzi.
Akiwa Zahanati ya Nyamalilo,Waziri Ummy amebaini kuwa
licha ya TAMISEMI kupeleka fedha za kukamilisha Zahanati hiyo Shilingi Mil 50 ambazo
kwa hali ya Zahanati ilivyokua ingekamilika na fedha kubaki lakini Viongozi hao
wa Kijiji waliendelea kuwachangisha wananchi sh 9,500 kwa Kaya kwa madai
wanakamilisha zahanati hiyo.
Viongozi wa kijiji cha Nyamililo wakiwa mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kuchangisha michango bila kibali. |
Wakiwasilisha malalamiko yao Wananchi hao wamesema
waliposhindwa kutoa michango hiyo walichukuliwa Kuku, mbuzi na wengine hata
Baiskeli kitendo ambacho hawakukifurahia na wao wanapenda maendeleo lakini
viongozi hao wa vijiji wamezidisha michango.
Akiwasilisha Taarifa ya Ukamilishaji wa Zahanati hiyo
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dr. Saumu Kumbisaga amesema ktk mil 50
zilizopokelewa wametumia sh Mil 33.2 na bakaa ni mil 16.7.
Kazi zilizofanyika ninupigaji wa ripu nje na na ndani, kukazia paa, uwekaji wa Fremu za madirisha na milango, uwekaji wa Gypsum board, kumwaga Jamvi, uwekaji wa vigae na ujenzi wa ukuta wa varander
Dr. Saumu.
Sanjari na hilo,Waaziri Ummy amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kumsimamisha kazi Mtendaji wa Kijiji cha Nyamiliho Mariam Mgunda kwa kuratibu zoezi la kuchangisha wananchi fedha.
0 Comments