WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu anawatangazia Wakurugenzi wote wapya 69
walioteuliwa kwa mara ya kwanza, kuripoti
Makao Makuu ya Ofisi za Rais –TAMISEMI – Dodoma tarehe 05.08.2021 kwenye
Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma – Mkapa House kuanzia saa tatu
asubuhi kwa ajili ya kupatiwa maelekezo mbalimbali.
Wakurugenzi hao wanatakiwa kuripoti wakiwa na cheti
cha kuzaliwa, Kitambulisho cha Tifa (NIDA),
Wasifu Binafsi (Cv), Vyeti vya Kitaaluma
pamoja na picha mbili (Passport Size).
Wakurugenzi ambao wamehamishwa vituo vya kazi na
wale walioendelea kuwepo kwenye vituo vyao vya awali, waendelee na utaratibu wa
kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya makabidhiano kuanzia
tarehe 03.08.2021
Halkadhalika Wakurugenzi ambao uteuzi wao
umesitishwa, wanatakiwa kwenda kuripoti kwa Makatibu Tawala wa Mikoa husika
mara moja.
0 Comments