📌 DOTTO KWILASA
AFISA Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa amewaonya
Maafisa biashara nchini wanaoghushi leseni na kutengeneza vitabu feki
kuacha tabia hiyo huku akisisitiza kuwa kitendo hicho kosa kisheria kwani
kinahujumu uchumi.
Hayo yamesemwa
Jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(Brela) Godfrey Nyaisa wakati akifungua mafunzo ya siku tano
kwa Maafisa biashara kutoka mikoa ya Morogoro,Singida na Dodoma kuhusu sheria
ya leseni za biashara.
Amesema,kuna
Halmashauri fulani(hakuitaja)Afisa biashara wake alifoji vitabu vya
risiti na mwisho wa siku alikamatwa jambo linaloleta aibu kwa jamii .
Maendeleo
hayataki uongo uongo ,kutokana na kuepukana na mambo kama haya tunataka kuweka
mfumo mzuri wa kuchukua vitabu na leseni kwa njia ya mtandao,njia hii
itakomesha wizi
Licha ya hayo
amewataka kuzingatia majukumu yao na kuepuka kuwa kikwazo kwa wafanya biashara
hali takayoleta mawasiliano mazuri baina yao na kutengeneza mtandao wa
maendeleo.
Amesema kuwa Maafisa
biashara wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwatembelea wafanyabiashara katika
maeneo yao na kuwapa elimu ya ulipaji wa kodi.
"Najua kunasheria
za biashara lakini wakati mwingine lazima muongozwe na busara ili kuweza kupata
matokeo yaliyo chanya,kwani kufunga biashara siyo suluhisho na pia ilishapitwa
na wakati"amesema Nyaisa.
Amesema,Serikali
haifanyi biashara ila inatoa huduma hivyo kupitia mafunzo hayo anaamini Maafisa
biashara watabadilika na watapata fikra mpya ambapo wataenda kutumika katika
kuongoza biashara.
Kuna maafisa
biashara wanapiga sana hela,wawekezaji wanakuja lakini mnawapiga urasimu sana
wakati nyie ndio mlitakiwa kuwapa ushirikiano mkubwa
Alisema mojawapo ya
kazi ya Afisa biashara ni kuhakikisha eneo lake lina wafanyabiashara na wanafahamiana
,lakini utakuta wengine hawatafuti wawekezaji na hata wakija bado tena
wanawakandamiza.
Pamoja na hayo
Mtendaji Mkuu huyo amewataka kuwatembelea na kutoa elimu kwa wafanyabiashara
kwasababu wapo ambao wanafanya biashara bila kuwa na leseni kutokana na
kuogopa.
"Mfanya biashara
asipokuwa na leseni hawezi kuendelea kwani hatoweza kupata mkopo kutoka
bank,lakini pia hakuna biashara inayokuwa yenyewe bila mkopo hata kama una
mshahara bado haitoshi kuikuza biashara yako bila mkopo"amesema.
0 Comments