IMEELEZWA kuwa mradi wa
ujenzi wa kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi
eneo la Kasumulu unaojengwa na mkandarasi China Geo Engineering Corporation umefikia
asilimia 67.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2021.
Hayo yamesemwa mkoani
Mbeya na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, mara
baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo hicho unaojengwa kwa awamu tatu na unagharimu
kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 26.
Nitoe wito kwa mhandisi mshauri kuusimiamia mradi huu kikamilifu ili ukamililike kama ulivyopangwa kulingana na mkataba
Aidha, Naibu Waziri
Kasekenya amesema kuwa mpaka sasa mkandarasi hana madai yoyote anayodai
yatakayokwamisha utekelezaji wa mradi huo.
Mhandisi Mshauri wa
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Huduma ya Pamoja Mpakani (OSBP) katika eneo la Kasumulu
kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Daniel Mandari, akitoa
taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey
Kasekenya, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, mkoani Mbeya.
Mhandisi Mandari ameongeza
kuwa mkandarasi amekwishakamilisha kazi za uandaaji wa ushindiliaji matuta ya
karibu barabara zote na kwa sasa anendelea kukamilisha miundombinu ya mabomba
ya maji safi, taka, zimamoto kabla ya kuanza tabaka la lami.
Kwa upande wake,
Mhandisi Mshauri wa Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi
Daniel Mandari, amemueleza Naibu Waziri kuwa licha changamoto zilizoukabili
mradi huo kuchelewa kukamilika, mkandarasi amekwisha kamilisha ofisi za
wahandisi na maabara asilimia 100, ujenzi wa jengo la malori asilimia 80, Ghala
asilimia 85, jengo la mifugo asilimia 84, jengo la abiria asilimia 81, geti
namba 1&2 asilimia 75 na mizani asilimia 85.
Kukamilika kwa ujenzi
wa kituo cha huduma ya pamoja mpakani (OSBP) mpakani mwa Tanzania na Malawi
katika eneo la Kasumulu kutakuza uchumi wa nchi zote mbili.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
0 Comments