📌 MWANDISHI WETU
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy
Mwalimu, amezindua Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara
Vijijini na Mijini(TARURA) wenye thamani ya Sh.Trilioni 3.6.
Uzinduzi
huo umefanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa Mpango
huo unaanza mwaka huu 2021/22 hadi 2025/26.
Mhe.Ummy
ameeleza kuwa mpango huo utaongeza mtandao wa barabara kutoka kilometa 2,404.90
hadi 3,855.65, changarawe kutoka kilometa 29,116.57 hadi 102,358.14 na madaraja
kutoka 2,812 hadi 6,620 na fedha zitakazotumika ni Sh.Trilioni 3.6.
Mpango huu kwa miaka mitano unahitaji Sh.Trilioni 3.6 sidhani kabisa Rais Samia kama atashindwa kwa kuwa anauwezo wa kuzitafuta ndani ya miaka mitatu, twendeni tukaoneshe kazi yenye ubora na ufanisi
Waziri Ummy amesema serikali itaupatia Wakala huo magari 122 na mchakato wa kuomba ajira za Wahandisi unaendelea na wataajiri Maofisa manunuzi kwa ajili na kutoa ajira za muda.
Aidha Ummy, amesema kuwa kwenye miji hiyo zitajengwa kilometa tano za barabara ya lami huku akisema kuna andiko litaandaliwa kwa ajili ya miji ambayo haitapata.
Hata
hivyo Ummy ametoa angalizo kwa Wakala huo kuhakikisha kazi za ujenzi wa
barabara zifanyike kwa ufanisi kwa kuwa ni kipimo chao kwa watanzania.
“Tunataka
tuone tija katika suala zima la ukarabati wa barabara mijini na vijijini, ndugu
zangu mnakazi kubwa mwaka huu mmoja ndio mwaka wa kuwapima je, kile kisingizio
cha kuwa hamna fedha kilikuwa kisingizio au hamna uwezo na ubunifu na utashi wa
kazi mnazotakiwa kuzifanya,”amesema.
Amesema
matarajio ya serikali kwa Tarura ni makubwa sana hivyo wasiiangushe na waoneshe
kuwa ni taasisi sahihi ya kufungua barabara za mijini na vijijini.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, David Silinde, amesema TARURA katika
historia ya nchi kwa mara ya kwanza imetengewa fedha nyingi.
“Nipongeze
Bunge kupitia kwa Spika wetu Job Ndugai kwa kupitisha kiwango cha fedha,
ambacho Tarura itaweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, malengo na
mikakati tuliyojadili hapa itatekelezwa kama ilivyokusudiwa,”amesema.
Naye
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, amesema mkutano huo wa
siku wa tatu mbali na kuzindua kauli mbiu, watapitia utekelezaji wa Mkakati wa
kwanza wa miaka minne na kupitia Mkakati wa Pili wa mwaka 2021/22 hadi mwaka
2024/25.
Awali
Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff ,amesema katika utekelezaji wa
Mpango Mkakati kuanzia mwaka 2017 hadi Juni mwaka 2021, jumla ya Sh. trilioni
1.3 zimetumika kutengeneza kilomita 24,979.24, ambapo kilomita 955.35
zimetengwa kwa kiwango cha lami, kilomita 16,857.82 za kiwango cha changarawe.
0 Comments