NDUGAI AWATAKA WALIMU KUJIVUNIA KAZI YAO



📌MWANDISHI WETU

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amewataka walimu kujivunia kazi yao kwa vile ni moja ya kazi ambayo ni tegemeo katika taifa lolote duniani.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Walimu wenye ulemavu,lililoandaliwa na Chama Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) jijini Dodoma,Ndugai amesema mchango wa mwalimu ni mkubwa kwa kila mwanadamu.

Ualimu ni kazi muhimu katika jamii,mpo katika ya maendeleo yetu.Hata viongozi wakubwa msingi wetu kazi ya mwalimu

Spika Ndugai pia amewataka walimu hao pia kumshukuru Mungu kwa kile alichowajaalia kuliko kuanza kulalamika kwa ulemavu walio nao.

Shukuruni kwa kile mlichonacho kuliko kulalamikia Mungu kwa tusichonacho na ukiangalia kile usichonacho basi kila mtu atakuwa si mkamilifu.

Sanjari na hilo Ndugai amewataka walimu hao kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowawezesha kuongeza kipato ili kuepukana na mikopo yenye riba kubwa wanayochukua huko mitaani.

Ndugai amesema walimu wengi wapo katika matatizo makubwa kwa sababu ya mikopo inayoumiza ambayo hupelekea hadi kuweka kadi zao za benki kama zamana huko mtaani ili wapatiwe fedha za kutatua shida zao.



Naye rais wa CWT Mwalimu Leah Ulaya amewapongeza walimu hao wenye ulemavu kwa uvumilivu wao licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya kazi.

Mwl.Ulaya pia amewataka walimu hao kuendelea kuchapa kazi na kuendelea kuiamini CWT katika kutetea haki na maslahi yao.



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CWT Deus Seif amesishukuru serikali kwa hatua kubwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili walimu nchini lakini pia imeiomba kutoa posho maalumu kwa ajili ya walimu walemavu ili kujikimu kutokana na gharama za maisha zitokanazo na ulemavu wao.

Kuna walimu wenye ulemavu wameajiri wasaidizi,tunaomba serikali iwatambue wasaidizi hao ili kuwapunguzia mzigo walimu hao wenye ulemavu

Pia Katibu huyo ameiomba serikali kutoa ruzuku kwa wanafunzi walemavu ili kuwatia moyo katika kujiendeleza kuliko kuwakopesha mkopo wa kulipia ada za masomo kama ilivyo sasa katika elimu ya juu.

Baadhi ya Walimu wakiwa kwenye kokangamano hilo.


 


Post a Comment

0 Comments