📌DOTTO KWILASA
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imewakutanisha
viongozi wawakilishi wa Serikali ngazi mbalimbali,makundi ya kijamii
,Taasisi za dini,Umma ,binafsi na vyama vya siasa katika kikao cha pamoja kwa
lengo la uhamasishaji na utoaji wa elimu ya sensa ya watu na makazi
inayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 .
Akieleza umuhimu wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma,Anthony Mtaka amesema wameandaa kikao hicho na kuyashirikisha makundi
hayo ili kurahisisha utoaji wa elimu ya sensa kwa jamii huku akisisitiza kwamba
kwa kufanya hivyo zoezi hilo litafanikiwa kama inavyotarajiwa.
Kwa kutambua umuhimu wa zoezi hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George
Simbachawene amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi katika zoezi
la sensa ya watu na makazi
linalotarajiwa kufanyika mwakani ili
kuiwezesha Serikali kupanga maendeleo na kukuza uchumi.
Akiongea katika kikao hicho amesema
Serikali inategemea sana zoezi hili,hatuwezi kuwa na maendeleo bila kujua idadi ya watanzania,kila mmoja kwa nafasi yake anatapaswa kuwa balozi wa uhamasishaji ni muhimu hivyo watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuisaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo
Mbali na hayo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka kwa kuona haja ya kuandaa mkutano huo huku akisisitiza kwamba sensa ni muhimu kwani inaleta ushahidi wa kisayansi na maendeleo.
Naye Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la
Kongwa,Job Ndugai amesema zoezi hilo ni
muhimu kwa Taifa kwani litasaidia Nchi kupanga maendeleo hivyo watanzania
wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
Tarehe 31 vikao vyetu vya Bunge vitaanza na vikao vilivyopita tumepitisha mambo mengi ikiwemo na tozo,safari hii itakuwa salama,hili ni jambo muhimu sana hivyo niwaombe watanzania wajitokeze kwa wingi,sisi wagogo hata zoezi la kuhesabu mifugo linakuwa na shida
ni utamaduni wetu.
Naye Kamisaa wa Sensa nchini ambaye pia ni Spika wa
Bunge Mstaafu,Anne Makinda ametoa wito kwa watanzania kujitokeza katika zoezi
la kuhesabiwa kwani hilo sio suala la kisiasa na kwamba zoezi hilo watatumia tehama katika maeneo ya
kuhesabiwa lengo likiwa ni kuwafikia watanzania wengi ambapo amedai watawafikia
watu wengi mpaka katika maeneo ya vijijini.
0 Comments