📌MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Dkt.Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wote wanaofanya kazi katika Taasisi zote
zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wajiandae kisaikolojia kupitia
mfumo wa mafunzo ya Kijeshi
Ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo Jijini Arusha ikiwa ni ziara ya kikazi Chuoni hapo ya kuwatembelea na kuzungumza na Watumishi hao ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi
Amesema mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia kwenda katika mfumo wa Jeshi Usu, yanalenga kuleta suluhisho la kudumu katika kukabiliana na changamoto za usimamizi wa rasilimali misitu na nyuki pamoja na wanyamapori nchini.
Amesema hakuna Mtumishi yeyote wa Taasisi hizo atakayekwepa mafunzo hayo kwa vile hiyo ni sera ya Wizara huku akisisitiza kuwa hilo halikwepeki na yeyote ambaye hayupo tayari basi ahame wizara hiyo ndiyo itakuwa salimika yake
Leo unaweza kuhamishwa kutoka Olmotonyi kwenda Shirika la Hifadhi za Taifa ( TANAPA) au TFS wenzako kule washakamilika tayari ni wanajeshi, wewe utakuwa raia
Amesisitiza kuwa kila mtumishi aliyeko katika Taasisi hizo lazima apitie mafunzo hayo kwa sababu watakuwa wakihamishwa kutoka Taasisi moja hadi nyingine ndani ya Wizara hivyo endapo hajapitia mafunzo hayo itamuwia vigumu katika kutekeleza majukumu yao wakati akiwa raia katika mfumo wa kijeshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza mwishoni mwa wiki na Wajumbe wa Menejimenti ya Chuo cha Misitu cha Olmotonyi |
Amezitaja Taasisi hizo kuwa ni Mfuko wa Misitu Tanzania (TFF) Mfuko wa Wanyamapori Tanzania ( TWPF) Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) Chuo cha Taifa cha Utalii ( NCT) Chuo cha Misitu Olmotonyi, Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Makumbusho ya Taifa (NMT), ChUo cha Nyuki Tabora (BTI), Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Taasisi ya Utafirti wa Misitu (TAFORI) TAWA, TANAPA na TFS
Kupitia agizo hilo,Dkt.Ndumbaro amezitaka Taasisi hizo kujiandaa kushiriki katika mafunzo hayo ambapo amesema mafunzo hayo yatatolewa kwa awamu awamu.
Akizungumza na Watumishi hao wa Chuo cha Olmotonyi, Dkt.Ndumbaro amesema anataka wanavyowafundisha wanafunzi wao ambao wataajiriwa TFS inayoendeshwa kijeshi ni lazima wakufunzi wao wawe wanajeshi kwanza
Haiwezekani mnawafundisha Wanafunzi waende kuajiriwa huko TFS kama wanajeshi wakati ninyi sio wanajeshi, mnawafundisha nini
Awali, Kamishna Uhifadhi wa TFS, Prof.Dos Santos Silayo alieleza kuwa kwa vile TFS ndo imekuwa muajiri mkuu wa Wahitimu wa Chuo hicho hivyo wameanza utaratibu wa kuhakikisha baadhi ya kozi katika Chuo hicho ziwe na mafunzo ya kijeshi ili kuwaandaa wanafunzi wa Chuo hicho wanapoajiriwa na TFS
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (
katikati) akimsikiliza Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania( TFS) Prof.Dos Santos Silayo ( kulia) wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya
katika Chuo cha Misitu cha Olmotonyi kilichopo Jijini Arusha
kuhakikisha hilo
linafanikiwa wao kama TFS imekichagua Chuo hicho kuwa mojawapo ya kituo cha
Mafunzo ya kijeshi kwa baadhi ya Maafisa kutoka TFS.
0 Comments