📌FAUSTINE GALAFONI
MKUU wa Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri ameagiza ujenzi wa mradi wa hoteli ya jiji la Dodoma inayojengwa mji wa serikali Mtumba ijulikanayo Government City Compex Hotel uwe ukamilika ifikapo tarehe 31,Agosti,2021.
Shekimweri ametoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki
akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeo ya ujenzi wa kitego uchumi hicho cha
jiji la Dodoma ambao umegharimu takriban Tsh.bilioni 18
fedha zitokanazo na mapato ya ndani.
Mkuu huyo wa wilaya amesema hoteli hiyo itakapokamilika itasaidia kuingiza mapato ya Tsh.bilioni 1.3 kwa mwaka sawa milioni 108 kwa kila mwezi hivyo unapochelewa kukamilika unapoteza mapato ya Tsh.Milioni 108 kila mwezi na hadi sasa jumla ya Tsh.Milioni 864 zimepotea kutokana na kuchelewa ambapo ulitarajiwa kukamilika mwaka jana.
Vile mnavyochelewa kumailizia ujenzi ndiyo mnavyodhidi kupoteza mapato,kwa sababu hadi sasa mmetoa tu lakini hamna dalili kuirudisha fedha ya wananchi kwa sababu mmechelewa kumaliza ujenzi.
DC Shekimweri akikagua moja ya chumba cha hoteli iliyopo katika kitega uchumi hicho. |
Mstahiki Meya wa
jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe amemuonya mkandarasi wa jingo hilo kuendelea
kufanya kazi kwa weledi na ubora hili kitega uchumi hicho kiltie matokeo
yaliyokusudiwa na halmashauri ya jiji la Dodoma.
Prof.Mwamfupe
alisema uharaka wa ujenzi huo usiathiri ubora wa umaliziaji wa jengo hilo
ambalo taratibu zote za malipo kwa mkandarasi zilishakamilika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi [CCM]Wilaya
ya Dodoma Meja Mstaafu Johnick Risasi akisema suala la mkataba linatakiwa
kuangaliwa upya ili kuondoa mkanganyiko pindi panapotokea ucheleweshaji wa
miradi.
Risasi alisema kila upande lazima uheshimu mkataba ili kutumiza malengo ya
miradi hiyo kwa muda uliowekwa.
Awali akitolea maelezo juu ya mradi huo ,msimamizi wa
ujenzi katika hoteli hiyo ya kisasa mji wa serikali yenye hadhi ya nyota
tano,mhandisi Nasri Nasoro kutoka kampuni ya M/S MOHAMMED BUILDERS
CO.LTD inayotekeleza mradi huo amesema ujenzi wa Hoteli hiyo umefikia
asilimia 75.
0 Comments