BASHE APIGA MARUFUKU 'UBABE' UKAMATAJI WA MAGARI YA MAZAO SHINYANGA

 


📌FAUSTINE GALAFONI

NAIBU Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema mkoa wa Shinyanga unaenda kinyume na Maelekezo ya wizara kwa kukamata magari yanayobeba mazao ya dengu ,kunde na mbaazi hivyo wanatakiwa kuacha mara Moja kamatakamata hiyo .

Bashe ametoa maagizo hayo leo Agosti 27,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo  amesema kuanzia leo magari yote yaliyokamatwa katika mkoa wa Shinyanga yaachiwe mara Moja hivyo amesema kitendo hicho kinachofanywa na uongozi  wa mkoa wa Shinyanga ni Cha kibabe.

Aidha,Bashe amesema mwenye mamlaka ya kuagiza zao liuzwe kwa namna gani katika minada ni Waziri wa Kilimo pekee.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara  Wana leseni lakini wanapofika katika mkoa wa Shinyanga wanakamatwa .



Wafanyabiashara wamelipa ushuru Simiyu lakini wanakamatwa Tinde ,hatutaki namna hii

Hata hivyo ,Bashe amesema halitajirudia lililotokea Shinyanga huku akiwapa pole wakulima pamoja na wafanyabiashara waliopata kadhia hiyo.

Zaidi ya Magari 30 ya mazao mbalimbali yalikamatwa mkoani Shinyanga kwa madai ya kutolipa ushuru wa mazao licha ya kulipa katika mikoa mingine 

 

Post a Comment

0 Comments