📌DOTTO
KWILASA
SERIKALI imewashauri wakulima
kutumia mbolea aina ya NPS na NPS ZIN-N.K kupandia mazao ambapo
gharama yake inatajwa kuwa ni ahueni ikilinganishwa na mbolea ya DAP ambayo
hutumiwa na wakulima wengi huku bei yake ikiwa juu kwenye soko la dunia
na kuwa kikwazo kwa wakulima wa hali ya chini.
Hatua hii imekuja kutokana
na malalamiko mengi ya wakulima kushindwa kumudu gharama za mbolea na
kusababisha kushindwa kuendeleza kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa Taifa
huku ajira nyingi za vijana zikitokana na sekta hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari
Jijini hapa, Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda amesema mbolea zote hizo za
aina tatu zinatumika kupandia mazao lakini kwa sababu moja kati ya hizo
gharama yake iko juu wakulima wanapaswa kutumia inayoendana na hali yao
kiuchumi.
Amefafanua kuwa Mbolea ya DAP
kwenye madukuka ya Dar es Salam Kg 50 inauzwa sh. 75,000 na bei yake
inaongezeka kwa mikoani hadi kufikia 100,000 bei ambayo inawaelemea
wakulima.
Amesema”Tumezungumza na watu
wanaoagiza mbolea ya NPS na NPS-ZINK ambao shehena wanayo na
wataongeza nyingine ambayo watauza 60,000 kwa mfuko wa kg 50 ambayo
ni sawa na bei ya mbolea ya mwaka jana na kwa sababu mbolea ni ya kutosha
tunahakikisha bei ya aina hii ya mbolea haitapanda tena,”amesema.
"Hatua nyingine
tutahakikisha mbolea inayokuja nchini ikifika bandalini inashushwa mapema na
kupelekwa kwenye maeneo husika hali hiyo itasaidia kupunguza gharama za
bandarini ambazo zilikuwa zinasababisha kuongeza gharama ya mfuko wa
mbolea,"amefafanua.
Mbali na hayo amebainisha kuwa
Wizara hiyo imeamua kukutana na wafanyabiashara wa mbolea nchini kwa
lengo la kukubaliana kuagiza mbolea kwa pamoja ili kupungiza gharama za
usafirishaji.
“Nampongeza waziri anayehusika na
mamlaka ya bandari kwa kutuhakikishia kuwa mbolea inapofika bandarini
haicheleweshwi,unapoagiza mzigo mkubwa wa mbolea hata gharama inapungua na
kutoa kibali kwa mamlaka ya mbolea kutoa vibali vya uagizaji mbolea ili wadau
wengi waweze kushawishika na kuagiza,”amesema Mkenda.
"Wakulima wasiwe na hofu
kwani serikali ni sikivu na itahakikisha inafanya kila jitihada ili wakulima
waendelee kuzalisha,"amesema.
Kutokana na hayo,Mkurugenzi wa
Kituo cha Utafiti wa Kilimo(TARI) Cha Mlingano Tanga Catheline Senkoro
amesema mbolea ya NPS na NPS-ZIN-N.K tayari imeshafanyiwa utafiti
na inafanya vizuri na tayari imeonyesha matokeo chanya kwenye mikoa ya nyanda
za juu kusini.
Ameongeza kuwa "Wakulima
wengi wamezoea kutumia mbolea ya aina moja ya DAP ambayo kwa sasa bei yake iko
juu na wakulima wengi watashindwa kumudu gharama,nawatoa hofu wakulima mbolea
hizi ni nzuri na zimefanyiwa utafiti kwenye mikoa ya iringa, njombe na
songwe,"amesema
0 Comments