📌NTEGHENJWA HOSSEAH
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ametoa siku 7 kwa vyombo vya Ulinzi na
Usalama kuchunguza vifo vya wanafunzi 3 waliofariki kwa kufunikwa na kifusi
katika Shule ya Msingi Mbori, Kata ya Motondo Wilayani Mpwapwa.
Wakati huo huo Mhe. Ummy amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma kuwaondoa Walimu wote wa shule ya Msingi Mbori kupisha uchunguzi unaondelea.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati aliposhiriki
kuaga Miili ya wanafunzi 3 waliofariki kwenye ajali ya kufukiwa na Mchanga
katika shule ya Msingi Mbori tarehe 27.07.2021.
Akiwa shuleni hapo Waziri Ummy amelaani vikali
Vitendo vya Walimu kuwafanyisha kazi siziso stahili za wanafunzi tofauti na
ilivyoelekezwa kwenye Waraka wa Elimu bila Malipo No. 3 wa Mwaka 2016.
Amesema “ Hatukatazi mwanafunzi kufanya kazi
zinazomjenga kama vile Stadi za kazi lakini sio kumfanya mwanafunzi kama
Kibarua unawezaje kumwambia mtoto akachimbe mchanga wa kujengea au akaponde kokoto tena bila uangalizi wa Walimu “ Alihoji
Katika Shule ya Msingi Mbori tumeleta sh. Mil.12 kwa
ajili ya Ujenzi wa Choo na fedha za mchanga zimejumlishwa humo inakuwaje walimu
watume watoto kwenda kuchimba mchanga wa mtoni, kuna uzembe hapa umefanyika na
tutachukua hatua.
Pia Waziri
Ummy aliwataka Wakuu wa shule zote Nchini na walimu wa ujumla kuacha
kuwatumikisha wanafunzi wawapo shuleni na wazingatie Waraka wa Elimu bila
Malipo no 3. wa mwaka 2016 ambao unatoa ufafanuzi wa kina wa jukumu la kila
mdau wa Elimu.
Jukumu la Ujenzi wa Miundombinu ya shule ni la Wazazi pamoja na Jamii inayozunguka na sio wanafunzi, Walimu na Kamati za shule mnatakiwa kuhamaisha Wazazi na jamii kujitolea kujenga miundombinu hiyo na sio kutumikisha wanafunzi
Waziri Ummy.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Josephat Maganga
amesema watoto waliofariki kwenye ajali ya kufukiwa na kifusi shuleni
hapo ni watatu ambao ni Isaya Lucas Hamis, Rehema Alex na Daud Enock Mchea na
watoto wengine watano walijeruhiwa wametibiwa na kuruhusiwa kurejea majumbani
kwao.
0 Comments