📌MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.
Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa wananchi kuendelea kufanya uhakiki wa laini
za simu kwa lengo la kutambua laini zilizosajiliwa kwa majina yao ili kuepuka
kuhusishwa na makosa ya utapeli mitandaoni.
Hayo ameyazungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa tovuti
na Mpango mkakati wa Wizara hiyo wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021/22 hadi
2025/26 uliofanyika jijini Dodoma
Amesema kuwa ni
muhimu kwa kila mwananchi kuepuka kusajili laini kwa kuweka alama ya kidole zaidi
ya mara moja ili kuzuia usajili wa laini nyingine za ziada ambazo zinaweza kutumika
kufanya uhalifu mitandaoni
“Wananchi wengi wamekuwa wahanga wa utapeli mitandaoni
hivyo Wizara imejipanga kuimarisha mifumo ya kulinda faragha na taarifa binafsi
ili zisitumike vibaya na watu wasiokuwa na nia njema”, alizungumza Dkt.
Ndugulile
Aidha, amewaasa wananchi kuacha kutoa taarifa binafsi au
kufuata maelekezo yeyote kwa watu wanaopiga simu na kujitambulisha wanatoka dawati
la huduma kwa mteja katika makampuni ya simu ili kuepuka kutapeliwa
Ameongeza kuwa namba wanayotakiwa kupigiwa na
makampuni ya simu ni namba 100 na sio kupigiwa na namba kutoka mitandao tofauti
na mitandao wanayotumia huku wakijitambulisha wametoka huduma kwamteja na
kuomba taarifa zao za kifedha au kutaka kujua salio lililopo katika laini zao
za simu.
0 Comments