📌DOTTO KWILASA
KUTOKANA na maendeleo ya TEHAMA nchini, uchumi wa kijiditali umekua kwa kasi na kurahisisha huduma za mitandao ambapo vitu vingi hasa bili za maji, luku na malipo ya ardhi yanafanyika kwa njia ya mtandado.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustin Ndugulile amezungumza hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa tovuti ya wizara hiyo na mpango mkakati wa wizara wa miaka mitano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini hapa.
Dk.Ndugulile amesema,Mpango huo unaifanya Tanzania kujiandaa kuingia katika hatua nzuri ya mapinduzi ya nne ya viwanda yatakayotoa mafanikio mazuri kwa uchumi wake.
Licha ya hayo ameeleza mwelekeo wa wizara hiyo kuwa ni kuwafanya Watanzania wote kuishi katika uchumi wa kidijitali kwa kufanya biashara zao kwenye mtandao.
Aidha amesema uchumi wa kidijitali unaondoa biashara ya flemu za maduka kwa kuwa muuzaji hatakuwa na haja ya kuweka bidhaa zake dukani na badala yake atauza kwenye mtandao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Zainab Chaula amesema wizara hiyo imejipanga kuongeza mfumo wa mawasiliano na kuachana na utaratibu wa kila wizara kuwa na mfumo wake wa mawasiliano.
Alisema hata Rais Samia Suluhu Hassan alishangazwa na kila wizara kuwa na mfumo wake na kutaka mfumo wa uwe mmoja kwa ajili ya kuongeza ufanisi.
Pia Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso alisema wabunge wako pamoja na
wizara hiyo na aliomba iliboreshe TTCL ili iweze kusimama na kutoa gawio kwa
Serikali.
0 Comments