📌DOTTO KWILASA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amewataka Viongozi wa Serikali kusimamia vyema rasilimali za Taifa kwa kuzingatia misingi ya uongozi na kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.
Ndugai ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa Mafunzo ya Uongozi ya siku nne kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.
Akiongea katika mkutano huo amewashauri Wakuu wa Mikoa na Makatibu tawala kuacha kulewa madaraka na badala yake watumie uongozi wao kusimamia miradi ya maendeleo na kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni na sheria.
Licha ya hayo amesema ni vyema
Viongozi hao wakafanyie kazi mafunzo hayo kwa kuepuka
majivuno na kuwanyanyasa walio chini yao bali kutenda haki kwa bila
kujali maskini au matajili huku wakizingatia miiko ya uongozi na mipaka
ya kazi yao huku akisisitiza kuwa cheo ni dhamana.
Kasimamieni sana shughuli za maendeleo na bajeti ya serikali, na maendeleo ya watu wenu kuanzia ngazi ya kaya na familia kwani maendeleo ya wananchi hayawezi kuja yenyewe yatatokana na ubunifu wenu na imani yenu kwao
Spika Ndugai.
Spika Ndugai pia amewashauri wateule hao Kujihusisha na masuala ya kilimo kwani kuna aina na mifumo mingi ya kufanya au kuendesha shughuli hiyo kwa njia ya kisasa na kupata kipato kinyume na Kilimo kilichokuwa kinafanyika zamani.
"Kilimo chetu kimekuwa chenye tija na Kilimo cha kuzoeleka kimeanza kupotea sasa mkaweke nguvu kusukuma gurudumu hili lifike mahali panapo stahili,
Kiongozi mzuri akiongea ,watu humsikiliza ,mkianza ninyi kama mfano na wananchi mnaowangoza itakuwa rahisi kuwaelekeza kwa vitendo, Lazima ninyi mkajenge misingi inayotakiwa ili wananchi wenu wapate maendeleo kupitia kilimo, mifugo uvuvi na huku ninyi mikiwa mstari wa mbele kuzifanya shughuli hizo,"amesema
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amesema mafunzo yaliyotolewa na taasisi ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala yatawasaidi kuboresha utendaji kazi wao na kuijenga Tanzania mpya.
Alisema mafunzo hayo yamechukua siku nne kwa wakuu wa mikoa 26 na yamegusa sehemu za msingi ambazo zitawasidia katika maeneo yao ya kazi na kuimarisha uhusiano kati ya viongozi wa mkoa na wale wa kitaifa
"Niwapongeze Sana taasisi ya uongozi kwa kuandaa mafunzo ambayo naamini yataleta chachu ya mabadiliko kwa wakuu na mikoa katika maeneo yao ya kazi pia nawapongea wakuu wa mikoa kwa kuonyesha ushirikiano kuanzia siku ya kwanza hadi mafunzo yalipofika tamati" alisema
Kwa upande wake Mwakilishi wa Taasisi ya Uongozi Zuhura Muro amesema hadi sasa taasisi hiyo imeweza kuwafikia viongozi zaidi 7000 wakiwemo wakuu wa mikoa, matibu tawala na watendaji wa halmashauri.
Kutokana na hatua hiyo ameipongeza Ofisi ya utumishi wa Umma kwa kuwezesha mafunzo hayo kwani ni sehemu ya maagizo yaliyotolewa na waziri Mohmed Mchengelewa ambaye aliiagiza taasisi kuwafikia viongozi wa umma .
"Mafunzo haya ya wiki nzima yamepata fursa ya kutoa mada 10 ambazo ni uongozi binafsi, itifaki, maadili ya uongozi na rushwa, usuruhishi wa migogoro, muundo wa serikali kuu, mahusiano yenye Tija, mahusiano ya kisekta, usimamizi Fedha, usimamizi wa miradi na usimamizi wa rasilimali za umma,
Ameongeza kuwa "Tunaishukuru TAMISEMI kwa kuona umuhimu na kuwezesha mafunzo haya kwa kada hii muhimu na wizara zote zilizofika na kutoa mafunzo mbalimbali ya kisekta ambayo yataleta mabadiliko makubwa kwenye utebdaji," alieleza
Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martini Shigela alisema wanamshukuru Rais Samia kwa kuwaamini na kuwapa nafasi miongoni mwa wengi na kumuhakikishia kuwa watawatumikia wananchi
"Nawapongeza washiriki kwa
kuonyesha moyo na dhamila ya kujifunza kwani toka mafunzo haya yaanze kila
mshiriki alikuwa anashiriki kwa asilimia zote, na kutokana na mafunzo haya
tunaahidi kuyatekeleza yote na kati yetu hakuna jambo baya litajitokeza
miongoni mwetu,"amesema.
0 Comments