📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
HAYO yamebainishwa Julai 2,202
jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda
wakati akifungua kikao cha kupata maoni ya wadau katika
mapitio ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 uliokutanisha Wabunge,Wenyeviti
wa Halmashauri ,Wanahabari ambapo amesema kumekuwa na udhaifu
katika sheria hiyo kwani umri wa serikali ni miaka 18 lakini vifungu vya sheria
ya ndoa Na.13 na 17 ya mwaka 1971 vinaruhusu mtoto kuolewa chini ya umri wa
miaka 18 .
Amesema wameanza mchakato wa kutekeleza uamuzi wa Mahakama kuu katika shauri Na.5 la mwaka 2016 na uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika Rufaa Na.204 ya mwaka 2017 kuhusu vifungu vya 13 na 17 vya Sheria hiyo vinaruhusu mtoto kuolewa chini ya umri wa miaka 18 kuwa ni kinyume na katiba ya nchi.
Tunaingia kwenye mjadala mkubwa na ninyi tunawashirikisha kama Wanachi wa Dodoma kwaajili ya kupitia na kupata namna ya kuitengeneza hii sheria ,kumekuwa na udhaifu katika sheria hii ,umri unaotambulika na serikali ni 18 lakini kwenye vifungu hivi vinasema anaweza kuolewa chini ya umri wa miaka 18 ambayo ni miaka 14 na 15 kwa majadiliano ama ridhaa ya wazazi
Pinda.
Pinda amefafanua kuwa
inapaswa kutafuta kitu ambacho kitawalinda watoto mpaka pale watakapofikisha
umri wa miaka 18’’Unaweza kuona mtihani tulionao tunatakiwa kutafuta kitu
ambacho kitawalinda, lakini vipi kwa wale ambao hawasomi tunapaswa kuwalinda
pia ili wanapotaka kuolewa wawe wamefikisha umri wa miaka 18’’amesema Pinda.
Pia amesema wakati mwingine
watoto huozeshwa katika umri mdogo hali inayopelekea kushindwa kuhimili ndoa
wakiwa na umri mdogo’’ ndiyo maana Majaji wametuambia tutafute namna nzuri ya
kuwaelekeza hawa watoto,tunahitaji mawazo juu ya sheria hii, tuko hapa kupokea
maoni yenu mbalimbali kuhusiana na hii sheria ilil isilete madhara kwa watoto
na lazima iboreshwe’’amesema Pinda.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Katiba na Sheria Amon Mpanju amesema wanachohitaji ni kupatikana kwa haki
ambayo itawasaidia wanachi kupata haki katika mifumo ya utoaji haki
’’tunahitaji Kulinda haki za wanawake na watoto wakike katika mifumo ya utoaji
haki hasa kwenye sheria hii ya ndoa,tunachohitaji ni maoni kutoka kwa wadau
kuhusiana na sheria hii’’amesema Mpanju
Msahiki Meya wa jiji la Dodoma
Prof.Davis Mwamfupe amependekeza kuwa mtihani wa Darasa la saba usiwe wa mwisho
bali uwe mtihani unaotoa njia panda mtoto mwingine anaenda vyuo vya ufundi na
mwingine anaendelea na sekondari.
‘Kwa kufanya hivyo tutamlinda
zaidi mwanafunzi na kumwongezea maarifa zaidi’amesema.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Chemba Comrade Sambala amesema si kweli kuwa makabila yote yanalingana
maumbile hivyo suala hilo ni la kuangalia kwa upana zaidi.
Mkuu Maendeleo ya jamii
halmashauri ya jiji la Dodoma Sharifa Yusuph amesema kuna haja kubwa kwa
sheria kufanyiwa mabadiliko kwani mtoto aliyechini ya umri wa miaka 18 hawezi
hata kufanya uchaguzi huku mhariri wa Tanzanite Selina Mathew akisema mtoto
chini ya umri wa miaka 18 hawezi kuhimili tendo la ndoa ambapo Mtangazaji
kutoka Azam Tv Joyce Mwakalinga akisema ni muhimu sheria mpya kufanyiwa
mchakato mapema.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini Antony Mavunde amesema ndoa za utotoni zimekuwa zikikwamisha maendeleo ya
mtoto wa kike hivyo anaungamkono uamuzi wa mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri
wa miaka 18.
Naye Mbunge wa jimbo la Mvumi Livingstone
Joseph Lusinde amesema ujenzi wa Taifa bora ni lazima uanzie
katika ngazi ya kaya.’’hivi ni kweli mtoto haelewi si kweli haelewi ,hawa
watoto wanaanza wakiwa na umri gani,tusianzie kwenye sheria tu ni kuanzia ngazi
ya kaya ,napata shida sielewi tunataka kupata nini,sheria hii inapingana na
mila na desturi,utafiti unasemajie tumefanya ya kutosha kuhusiana na matatizo
makubwa tuliyonayo ili nchi ikawe sawasawa,nashauri mila na desturi zetu
ziimarishe suala la watu kuoana hata wazazi hawahusiki,tusiweke sheria ambayo
itatukosanisha na watu ‘’amesema Lusinde
0 Comments