📌ALEX SONNA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka amewataka vijana wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanakuwa na
ujuzi ili kwendana na kasi ya Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.
Akizungumza leo,Julai 22,2021,katika mahafali ya
tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre(Dodoma VCT)Mkuu huyo wa Mkoa
amewataka vijana wa Mkoa huo kuwa na ujuzi ili kuzikimbilia fursa mbalimbali
ambazo zitapatikana kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.
“Wito wangu kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma niwatake
kuwa na ujuzi katika Makao Makuu ya Nchi niwatake kila mmoja apate ujuzi
tumieni vyuo vya kati wazazi niwaombe watoto wapate ujuzi
kama hajafaulu apate nafasi ya kusoma ujuzi wowote, Dodoma na Dunia
tunayoiendea itakuwa na fursa nyingi lakini kama huna ujuzi utapishana na fursa
“Mtu anaenda Garage anakuwa ni msafisha vioo lakini
baadae anajifunza umakenika baadae anajifunza udereva anakuwa dereva,vijana
wengi ni bodaboda wewe (wahitimu) kuwa fundi bodaboda utakuwa
umepata ajira lazima vijana mhakikishe mna ujuzi na kuna kozi zingine ni fupi
tu”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Dodoma ni Makao Makuu hivyo mnafaida mjiandae miradi inayokuja ikukute una ujuzi hapa ujenzi ni mkubwa sana kama unakaa nyumbani hakuna kibarua ni wewe tu,tumia fursa.Tunajenga hapo Msalato likiwanja likubwa kabisa wakikuuliza una ujuzi wewe upo tu tafuta ujuzi.
Kama unakaa hapa usidhani unapoteza muda kuna siku
utamkumbuka huyu mama wazazi viombeeni hivi vyuo vya ujuzi kama kuna mtu
anakudanganya fundi amekosa ajira huyo anakudanganya.Kama unasoma ujuzi
shikilia hivyo ninyi hamjapoteza na wazazi mliopo nyumbani usikae na
mototo ambaye hana ujuzi.
“Nakuombea Madame kazi zote duniani tunaanzia chini
kazi moja tu ndio unaanzia juu kwenda chini kazi hiyo ni
kuchimba kaburi na hapa tumeanza.Endelea kusoma mazingira kozi gani
utaziongeza ili washindane na tembelea vyuo vingine uone ambavyo wanavyo wewe
huna na mitaala pamoja na walimu,”amesema
Mkuu huyo wa Mkoa pia amekitaka Chuo hicho kuongeza
ubunifu pamoja na kozi mbalimbali ili watu wengi waweze kupata
ujuzi ambao utasaidia kuondokona na changamoto ya ajira.
“Madame nakushauru sana ongeza kozi
tujitahidi tuweke matangazo kwamba Chuo kinafundisha kozi hizi na hizi local radio
zungumza uwaokoe watoto wa Dodoma,tukitaka vijana wa Mkoa huu wawe washindani
tuwapeleke kwenye elimu zote ya darasani,ufundi,elimu dunia aghera.Dunia
tunayoiendea tunahitaji maeneo ya namna hiyo nimeona kozi zako ongeza kozi ili
watu wajifunze kuwe na ujuzi”amesema.
Pia,amewataka wanafunzi licha ya kujifunza masomo
mbalimbali pia wanatakiwa kuwa wabunifu ili wanapomaliza masomo yao waweze
kuajirika kirahisi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akigawa vyeti kwa wahitimu mbalimbali kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi
Kuhusiana na changamoto ya eneo la ardhi la chuo hicho,RC
Mtaka ameutaka uongozi wa Chuo kwenda makao makuu ya kata ili kukutana na timu
ambayo inazunguka Mkoa wa Dodoma kumaliza changamoto za migogoro ya ardhi.
“Mjifunze vyote ujuzi na ubunifu ukienda mahali
kutafuta vibarua unakuwa umekamilika kwa kila kitu,tunapeleka umeme vijiji
vyote vya Tanzania kule vijijini hakuna mafundi maana yake fundi ni
wewe.Tunapeleka umeme na maji katika vituo vya afya bomba likiharibika au
kuziba wewe ndio fundi,”amesema.
“Nikuombe kama utatumia nafasi
vizuri,wanalalamikiana waende makao makuu ya Kata ili waweze kulitatua.Nakuomba
uwezekutumia nafasi hiyo kupata muafaka katika siku hizo 10 ambazo tumeziongeza
kwani tulitenga siku 10 na tuliongeza siku 10 zingine,”amesema RC Mtaka.
Mkuu wa Chuo cha
Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi,akisoma risali wakati wa Mahafali
ya tano ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.
Awali akisoma risala Mkuu wa Chuo hicho,Jemima
Nchimbi amesema wanakabiliwa na changamoto kukosa eneo la kujenga chuo
kutokakana na eneo walilolipata kukabiliwa na mgogoro.
Amezitaja changamoro zingine ni vijana kutokupata
mikopo kwa kozi za ufundi stadi,uelewa mdogo wa wazazi kutambua kozi
zote ni kwa ajili ya jinsia zote.
Amesema mafanikio ambayo wameyapata ni pamoja na
kufundisha vijana 679 wa kozi fupi,kufundisha vijana wa kike na wa
kiume kwa kozi ndefu zaidi ya 333 ambapo vijana 1002 wameweza kupata mafunzo
ambapo asilimia 75 wameajiriwa na asilimia 25 wamejiajiri.
Vilevile,amesema wamefanikiwa wamefanikiwa kutoa
mafunzo kwa kina mama zaidi ya 197 kwa kozi za ujasiriamali na baadhi yao
wamefungua maduka na kuuza bidhaa walizojifunza kutengeneza.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka akikata keki
wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre
kilichopo jijini Dodoma.
0 Comments