📌DOTTO KWILASA
MKUU wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka
amesema Jamii ina jukumu la kujilinda yenyewe na kuwalinda wengine dhidi ya
ugonjwa wa COVID-19 bila kusubiri
kusukumwa.
Akiongea katika mkutano huo,Mtaka
amesema,uhai wa mtu sio Mali ya serikali hivyo ni jukumu la kila moja
kuhakikisha anajilinda kwa kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni,kuvaa
barakoa na kutumia vipupuzi.
Serikali ilishatoa miongozo mbalimbali ya kujikinga na janga la Corona lakini watu bado wanahoji kuitaka Serikali kutoa miongozo,mnataka miongozo gani hiyo!?
Mtaka,RC Dodoma
Pamoja na hayo Mtaka ameeleza miongozo na hatua kadhaa ambazo Mkoa wa Dodoma umeanza kuzifuata Katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo kwamba wao kama mkoa wamedhamiria kuanza na maeneo ya stendi,sokoni,minadani na sehemu zote zenye mikusanyiko.
Amesema,kulingana na mabasi ya abiria kujaza wasafiri , ipo haja ya kuboresha miundombinu hiyo ili kuendana na hali ilivyo ambao kila chombo Cha usafiri kitatakiwa kuwa na idadi ndogo ya abiria kwa kila safari kuepusha maambukizi.
"Wasafirishaji wa abiria mnatakiwa kuzingatia maeleko yote yanayotolewa na Wizara ya afya,hampaswi kusimamisha abiria ndani ya gari na hili tunaomba wafanya biashara wa magari mtuelewe vizuri," amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma.
”Hatuwezi kuzuia watu wasisafiri,hili haliepukiki sehemu yeyote hivyo ni vyema watu wakawa na mazoea ya kukubali kusafiri bila kubanana kwenye Vyombo vya usafiri,"amesema.
Kuhusu Masoko,Mkuu huyo wa mkoa ameagiza Wafanyabiashara wa Masoko yote yaliopo mkoani Dodoma,kuvaa barakoa kila wanapohudumia wateja wao ikiwa ni pamona na watoa huduma waliomo ndani ya eneo la solo kuhakikisha wanatoa huduma wakiwa wamevaa barakoa .
"Hatuwezi kufunga minada kwa sababu za ujinga wa wachache,kila mmoja anajua namna ya kujikinga,niwaambie tu kuwa mnada huu ndiyo utakuwa wa mwisho kwa ninyi kuuza bidhaa zenu bila kufuata Sheria za kujikinga na Corona,minada inayofuta baada ya leo tunataka kukuta kila mfanyabiashara maevaa barakoa,na hii ni lazima na sio ombi,"amesisitiza Mtaka.
Pia amehimiza Uongozi wa minada yote kuhakikisha minada inakuwa na huduma za maji tiririka,sabuni na vitakasa mikono kuwezesha wananchi wanaopata huduma kupata maji kwa urahisi kwa ajili ya kujitakasa.
Licha ya hayo ametoa wito kwa jamii kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya mara wanapoona dalili za ugonjwa huo ili kubaini huku akiwatahadharisha kuepuka kujifukiza bila utaratibu.
"Nipende kusema kuwa suala la Ugonjwa unaotokana na kirusi cha Covid -19 awamu ya tatu ni ugonjwa unaolikumba taifa kutokana na hali hiyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha analinda afya yake bila kusubili maelekezo ya kutoka ngazi ya taifa" alisema mwamfupe.
Kutokana na umuhimu huo,Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Njisia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima ametumia nafasi hiyo kuwata wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya nchini kuzingati miongozo 16 ya kujikinga na kupambana na ugonjwa wa Corona (CORONA 19 awamu ya 3).
Dk.Gwajima Kila mkoa unapaswa kujipambanua kuona namna ya kuwashawishi wananchi wake kuwa makini na ugonjwa huo hasa Katika kipindi hiki ambacho wagonjwa wa Corona wameanza kuonekana katika hospitali zilizopo hapa nchini.
"Kwa maana hiyo kama wilaya au mkoa tuone sasa tumejipanga vipi kukabiliana na janga hilo kubwa linaloitesa dunia zima.
Nimefurahi kuona mmejipanga katika mapambano ya Corona kila sehemu
lakini niwe muwazi nimekuwa nikipata Maoni mengi kwa wananchi waishio pembezoni
huko vijijini elimu ya kujikinga na kupambana na Corona haiwafikii,jitahidini
kwa hili
Dkt Gwajima.
Amesema vita ya ugonjwa wa Corona itakoma na kushindwa ikiwa wananchi watakubali kubadili tabia na kufuata miongozo inayotolewa na wizara ya Afya.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma, Meja Mstaafu Salingo Risasi amesema Viongozi wa Dodoma wamekuwa na ushirikiano mkubwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mapambano hayo ya Corona na wamekuwa wakikutana kwenye vikao katika kujadili namba ya wananchi kuweza kupata elimu ya kujikinga na ugonjwa huo.
0 Comments