📌 MWANDISHI WETU
VIJANA wa Tanzania
wanayo fursa kubwa ya kuchangia kwenye kutatua changamoto za mifumo ya chakula
kwa kutumia ubunifu, ujuzi na maarifa.
Ushauri huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe wakati
akifungua kongamanao la vijana kujadili mifumo ya chakula (Food System Summit) kwa
mwaka 2021 mkoani Dodoma.
Amesema suluhisho la
uhakika wa mifumo ya chakula unategemea sana ubunifu na ushiriki wa vijana
nchini ili sekta ya kilimo iwe endelevu na kuzalisha ajira kwa vijana
wanaojihusisha kwenye mnyororo wa thamani katika sekta ya Kilimo ..
Kwa upande wake Mshauri
wa Sera na Mratibu wa Mkakati wa Vijana kushiriki kwenye Kilimo toka Wizara ya
Kilimo Revelian Ngaiza alisema mkakati wa serikali unahusisha kuwajengea uwezo
vijana kuanzisha Kilimo biashara na kuajili wengine ili kuchangia
zaidi kwenye uchumi wa Taifa.
Serikali inawataka
vijana nchini kupitia kongamano hili
watoe mawazo katika kuboresha mifumo ya chakula itakayochangia kukuza
uchumi wa vijana na taifa kupitia sekta ya Kilimo
Ngaiza.
Akitoa mada kwenye
kongamano hilo Mtaalaam wa lishe kutoka Wizara ya Kilimo Magret Natai alisema Mifumo
ya Chakula inamaanisha kuwa “mkusanyiko wa shughuli mbalimabali zinazohusisha
uzalishaji wa chakula, kuanzia kwa mzalishaji (mkulima na mfugaji) ukijumlisha
wadau wa kati, wasambazaji ,wasindikaji, wasafirishaji mpaka mlaji” .
Naye mtaalam wa lishe kutoka Shirika la Mpango wa
Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Stella Kimambo akichangia kwenye
kongamano hilo amesema kuna umuhimu wa kubadili utaratibu wa uzalishaji na
matumizi ya ulaji vyakula vyenye kuzingatia lishe bora .
Wizara ya Kilimo
imepewa jukumu la kuratibu na kuhakikisha wadau wote wa sekta ya umma na binafsi
katika mfumo wa chakula wanashiriki mijadala ambapo mapendekezo ya nchi
yatawalishwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Septemba
mwaka huu New York Marekani.
0 Comments