📌ASILA TWAHA
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amewataka wafamasia kufuata maadili ya kazi
zao ili kulinda heshima katika kada husika.
Dkt. Magembe ameeleza hayo katika ufunguzi wa
mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa bidhaa za Afya kwa wafamasia wa Mikoa na
Halmashauri Julai 28, 2021 Jiji Dodoma.
Amesema wafamasia ni moja kati ya kada muhimu katika
sekta ya afya ambayo inahitaji watendaji waadilifu na wenye uaminifu katika kutekeleza kazi zao.
"Wapo baadhi ya wanataaluma wachache wasio waadilifu na wanaharibu kwa kutokuwa waaminifu na kuharibu taaluma hiyo ambayo inategemewa katika mchango mkubwa kwenye Sekata ya Afya. Amesema Magembe, nakuongeza
hata tukinunua dawa kiasi gani lakini kama hakuna usimamizi mzuri hatuwezi kupiga hatua
Katika hatua nyingine, ameweka wazi na kutoa maelekezo kupitia mafunzo hayo
kwakuwataka wataalam wote wa Afya
kuzingatia taratibu za serikali katika usimamizi wa bidhaa za afya na pale itakapobainika kuwepo na uzembe au ubadhilifu wa ukiukwaji wa taratibu,
kisheria na kanuni ambazo zinaisababishia serikali kupata hasara hatua kali zitachukuliwa. Amesisitiza
Ni jukumu la kila mmoja wetu aliyepo hapa kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora za dawa kulingana na miongozo ya tiba iliyopo
Dkt. Grace
Vilevile amewawataka wakaguzi na maduka ya dawa kuwa na wajibu wa kutoa taarifa kwa Baraza na mamlaka wanazoshirikiana nazo wakiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA) kuhusiana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo inayohusiana na utoaji wa huduma na utendaji wa taaluma iwe kwenye sekta binafasi au ya umma
Naye Masajili wa Baraza la Famasi nchini Bi.
Elizabeth Shekalaghe ameishukuru serikali kwakuongeza bajeti ya Afya na
kuwahimiza wafamasia kusimamia maadili na kuipenda kazi yao kwa kujitoa
kuitumikia vyema taaluma yao.
0 Comments