📌DOTTO KWILASA
SERIKALI imewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufuatilia kwa ukaribu migogoro ya ardhi na kuipatia ufumbuzi bila kusubiri viongozi wa ngazi ya kitaifa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amesema hayo wakati akizungumza na wadau wa Ardhi katika mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za mkuu wa mkoa.
Amewataka viongozi hao kuwajibika na si kusubiri viongozi wakubwa wafike waanze kusikiliza na kutatua migogoro wakati viongozi wa mikoa wa wilaya wapo itakuwa ni jambo la aibu, ni vyema mkaanza ninyi itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa asilimia 90.
Amesema serikali ina mpango wa kuanza kuwasajili madalali wa ardhi nchi nzima ili wafanye kazi kwa weredi huku wakilipa kodi
Hakuna kitu kinamuumiza mwananchi wa kawaida kama migogoro ya ardhi hivyo lazima viongozi wa mikoa na wilaya katika maeneo yenu kuhakikisha tunalinda rasilimali za maskini hasa ardhi
Pamoja na hayo amesema Jiji la
Dodoma linatakiwa liwe la kisasa ambalo halina migogoro ya ardhi ili wananchi
wake wajenge nyumba kwa kufuata utaratibu wa eneo husika ikiwa ni pamoja na
kuendeleza mji kwa kujenga nje kidogo ya maeneo ya mijini.
"Ningependa viongozi wa mkoa wajishughulishe sana kusikiliza kero za ardhi mkoa wa Dodoma wameanza ningependa mikoa yote Tanzania iige ianze kusikiliza kero pamoja na kuzia ujenzi holela wa makazi," ameeleza
Licha ya hayo amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Mijini kuacha kujihusisha kwenye masuala ya kuuza ardhi bali shughuli hizo zitasimamiwa na wakurugenzi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema katika kuhakikisha wanatekeleza agizo la Waziri huyo wa Ardhi ,Ofisi yake imetenga Siku 10 za kusikiliza kesi za migogoro ya ardhi kuanzia Julai 5 mwaka huu katika ukumbi wa jakaya kikwete.
Mtaka amesema katika siku hizo wametenga Siku tatu kwa ajili ya kusikiliza wananchi na kupokea malalamiko yao huku siku saba zitakuwa kwa ajili ya kufika kwenye maeneo yenye migogoro.
"Tunaelekeza nguvu kutatua migogoro ya ardhi hali hii itasaidia Wananchi kuishi kwa amani ,katika kutatua kero hiyo wananchi wafike na nyaraka zao zote na masharti ya wataaalamu wa afya yatazingatiwa kuhakikisha wanajikinga na maambukizi ya virusi vya Corona,"amesema na kuongeza;
Tunataka kuona Jiji la Dodoma linafanana na majiji mengine duniani ambako hakuna migogoro ya ardhi, hivyo wananchi watatakiwa kufika mapema kuanzia saa moja asubuhi
Kutokana na hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa amempongeza Waziri wa Ardhi kwa kuendelea kupambana dhidi ya migogoro ambayo ilikuwa imekithili na kusababisha baadhi ya shughuli za maendeleo kukwama.
Amesema migogoro ya ardhi inawavunja moyo wawekezaji na kuwataka wananchi kuzingatia utaratibu wa mipango miji ili jiji liwe la kisasa zaidi.
"Katika kutekeleza majukumu
nawashauri watumishi wa serikali wajipange kusikiliza kero za wananchi
kwasababu ni maagizo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya chama na
serikali kwa ujumla,"amesema
0 Comments