📌JOSEPHINE MAJURA, WFM
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaagiza watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha
kuwa hakuna Wizara ama taasisi itakayopelekewa chini ya asilimia 50 ya bajeti
yake ya maendeleo katika bajeti ya Serikali iliyooanza kutelezwa kuanzia Julai
mosi mwaka huu.
Ametoa Maagizo hayo wakati akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ametoa mwelekeo wa utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2022.
Nataka mkasimaie ugawaji wa rasilimaji fedha kwa kila Wizara ili tukirudi tena bungeni kuelezea utekelezaji wa bajeti kusiwe na mahali ambapo fedha za maendeleo zitakuwa zimepelekwa chini ya asilimia 50
Dkt. Nchemba.
Aidha, aliwaagiza watumishi hao kujiwekea
utaratibu wa kufuatilia kwa umakini utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
inayotokana na fedha zinakazotolewa na Serikali ili kuona utekelezaji wake na
kama zimetumika kama ilivyokusudiwa kwa kuwa itasaidia miradi kukamilika kwa
wakati.
Aidha, aliwataka watumishi hao kuendelea
kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia maadili, kanuni na taratibu za
Utumishi wa Umma.
Dkt. Mwigulu aliongeza kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan anaitegemea wizara katika masuala
yote ya uchumi hivyo ni jukumu la Wizara kuhakikisha inatoa ushauri mbalimbali
wa kitaalamu kuhusu masuala ya uchumi kwa maendeleo ya nchi.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Emmanuel Tutuba |
Vile vile Dkt. Mwigulu aliwataka watumishi
hao kuwa wabunifu hususan katika kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuisaidia
Serikali katika kukuza uchumi wa nchi.
Alitoa wito kwa watumishi kuendelea
kutumia fursa za mafunzo zilizopo ili kujiongezea ujuzi, lakini pia aliagiza
kuwepo na utaratibu mzuri ambao kila mtumishi atapata nafasi ya kuhudhuria
mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuongeza ujuzi kwenye taaluma zao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, aliwapongeza watumishi kwa ufanyaji kazi na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha jukumu la kusimamia uchumi wa nchi inatekelezwa kwa ufanisi zaidi.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia wakati wa kikao kazi na watumishi wa wizara hiyo. |
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba, alisema kuwa
Wizara inaendelea kusimamia uchapaji kazi, maadili na maslahi ya watumishi
ambapo watumishi wamepandishwa vyeo na kupandishwa madaraja.
Tumewandisha madaraja na kuwabadilishia miundo watumishi 529 baada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza watumishi wote wapandishwe madaraja wakati wa Siku ya wafanyakazi Mei Mosi na pia tumewathibitisha kazini watumishi 31
Bw. Tutuba
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia Utawala Dkt. Khatibu Kazungu alimhakikisha Waziri wa Fedha na Mipango kwamba atasimamia utaribu wa mafunzo kwa watumishi ili kuwajengea uwezo katika taaluma zao na kuwaongezea ufanisi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango anayeshughulikia Uchumi Bw. Adolf Ndunguru alisema kuwa Wizara
itaimarisha eneo la utafiti ili kuiwezesha Wizara kusimamia uchumi wa nchi.
0 Comments