📌ATLEY KUNI TAMISEMI
NAIBU KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, ameitaka Bodi ya
Mikopo ya Halmashauri kufanya tathmini ya kina kabla ya kutoa Mikopo kwa
Halmashauri hizo ili kufikia tija iliyokusudiwa.
Mweli ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipofanya
ziara katika Ofisi za taasisi hiyo iliyo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
kisha kufanya mazungumzo na uongozi na watumishi wa Taasisi hiyo, ambapo
aliwasisitiza watendaji katika Bodi kubadili mtazamo wa kiutendaji na kuja na
mawazo mbadala katika kuendesha Bodi hiyo.
Pamoja na mimi kuja kujua changamoto zinazowakabili, lakini mnachotakiwa sasa mbadilike na mfanye kazi kwa matokeo, wakati wa Uchambuzi wa bajeti (scrutinization), tutumie fursa hiyo kuzipima Halmashauri zile zinazo weza kufanya marejesho na zile ambazo zinasuasua katika marejesho
Alisema Mweli na kuongeza kuwa, lazima Bodi iwe na
ajenda, Je! Fedha zinazokopeshwa kwa Halmashauri, mradi husika utaweza
kurejesha fedha husika? Alisisitiza kwa kuhoji Mweli.
Mweli ameitaka Bodi kubadili mfumo wa kudai madeni,
na kuwataka kufanyia kazi yale yaliyo upande wao kama Bodi na yanayohitaji
maamuzi ya Wizara, yafikishwe Wizarani kwa hatua muhimu.
Awali akisoma taarifa ya Utendaji kazi, Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Yeremiah Titto Mahinya, alimwambia Naibu Katibu
Mkuu kuwa, dhumuni la Bodi hiyo nikuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa,
kufanikisha miradi ya maendeleo itakayowasadia katika kuinua mapato na kuchochea
shughuli za kiuchumi.
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa iliundwa chini
ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura ya 290 RE 2002, chini ya Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa aidha Bodi inaendesha shughuli zake
kwa mujibu wa Sheria iliyounda Bodi husika.
0 Comments