📌DOTTO KWILASA
SERIKALI imetenga kiasi cha Sh Bilioni 149 kugharamia bima za afya kwa wananchi wasio na uwezo hali itakayoboresha huduma za afya nchini,
Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hayo
wakati akizindua Bodi mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Maadhimisho ya
miaka 20 ya NHIF.
Amesema katika bajeti hiyo mpya ambayo utekelezaji wake umeanza leo Julai 1, Serikali ya Rais Samia itaendelea kuboresha sekta hiyo muhimu kwa mustakabali wa maisha ya Watanzania.
“ Utekelezaji wa jambo hili unaenda vizuri na kama mlivyomsikia Waziri Mkuu alipokuwa akisoma hotuba ya kuwasilisha hoja ya kuhitimisha bunge alisema serikali imejipanga kuwasilisha muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote kwenye bunge la Septemba mwaka huu
Waziri Gwajima amesema katika kusherekea miaka 20 ya kuanzishwa kwa NHIF kunatoa nuru kuanza kujipanga zaidi kuwafikia wanachama na kuwasikiliza mahitaji yao kwani itasaidia kuboresha zaidi na kuufanya mfuko kuwa bora zaidi.
Wekeni mipango madhubuti ya kushughulikia changamoto ambazo mmekabiliana nazo katika kipindi hiki ili ziwe chachu ya kufikia mafanikio na lengo la serikali ya kila mtanzania kuwa ndani ya mfumo wa bima ya afya.
Dkt.Gwajima
Licha ya hayo ameutaka mfuko huo wa NHIF kutumia kipindi hiki cha siku 90 za maadhimisho kutoa elimu zaidi na kuhamasisha wananchi hususani wa Vijijini ili waweze kuona umuhimu wa bima ya afya na kujiunga nayo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga amesema kwa kipindi cha miaka 20 ya utoaji huduma NHIF imeongeza wigo wa kutoa huduma kwa kuendelea kusajili vituo vya kutolea huduma za afya.
Amefafanua kuwa,mfuko umeongeza huduma kutoka vituo 3,198 wakati inaanzishwa hadi kufikia vituo 8970 juni Mwaka huu.
"Katika kupanua
wigo wa wanachama wetu, mfuko umejumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Wabunge, Wajumbe wa baraza la wawakilishi, Wajasiriamali, Wafanyakazi wa
Kampuni Binafsi na Wanafunzi wa vyuo,"amesema na kuongeza;
“Idadi ya wanachama na wachangiaji imeongezeka kutoka wanufaika 691,774 mwaka 2001 hadi kufikia wanufaika milioni 4.3 mwezi Machi 2021 sawa na asilimia nane ya watanzania wote,”Amesema Konga.
0 Comments