📌JOHN BANDA
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Selemani Jafo, amesema takwimu zinazotolewa na
Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu ni Muhimu kwa Sababu zimekuwa zikiisaidia
Serikali hususani Wizara yake kuchukua Tahadhari kuhusu suala zima la
Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Mito na Mabwawa.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma
kwenye Wiki ya mazingira alipotembelea Banda la Maoensho la Bodi ya
Maji Bonde la Wami Ruvu.
Amesema Rasilimali maji ni Muhimu kwa
maendeleo na Ustawi wa Binadamu, hivyo ameitaka Bodi hiyo ya Maji katika Bonde
la Wami Ruvu kuwa mstari wa Mbele kuiongoza Serikali kupitia Takwimu zake ili
iweze kuchukua hatua stahiki za kukabiliana na athari za Mazingira kwenye
vyanzo vya Maji.
Ofisi yenu ni muhimu sana, lakini inatusaidia vile vile kutoa tahadhari watu wasivamie vyanzo vya maji Kwa Sababu wakivamia Mambo yote yanakuja kuharibika, kwa mfano leo hii tunajenga lile bwana la Nyerere kama watu watavamia vyanzo vya Maji lile bwana litakuwa halijai
Waziri wan chi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo akiwa katika picha ya
pamoja na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu
Kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani
kinatarajia kufikia kilele chake June 5, ambapo Serikali inatarajia kuzindua
Kampeni Kabambe ya Kuhamasisha Jamii Kutunza na Kulinda Mazingira.
0 Comments