WAPIGA KELELE MITAANI SASA 'KIKAANGONI'

 

 


 ðŸ“ŒDOTTO KWILASA .

KATIKA kulinda afya ya jamii Kutokana na athari zitokanazo na kelele na mitetemo ,Serikali imeelekeza kuwa wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama inavyoelekezwa kwenye masharti ya leseni zao ikiwa ni Pamoja na  kila mwananchi kuhakikisha shughuli anazofanya hazisababishi kero ya kelele na mitetemo kwa jamii.

Hayo yameelezwa jijini hapa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano na Mazingira Seleman Jaffo wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira utokanao na kelele na mitetemo.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ongezeko kubwa la kelele na mitetemo na kusababisha kero inayopelekea jamii kukosa utulivu.

Kutokana na hayo Waziri Jafo amesema,ili kuleta utulivu kwa jamii wamiliki wa nyumba za ibada,kumbi za starehe na burudani wahakikishe sauti zitokanazo na shughuli zao hazizidi viwango vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria.

"Wananchi mnaombwa kutoa taarifa kuhusu kero ya kelele na mitetemo kwa Ofisi za Serikali za Mitaa au NEMC kwa namba za bure 0800110115 au 0800110117 na 08800110116,vilevile hakikisheni agenda ya kelele na mitetemo inakuwa kwenye mikutano yenu,"amesema

Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana ya usimamizi wa maziñgira amefafanua kuwa Pamoja na kuwepo kwa kanuni za usimamizi wa mazingira kwenye kitengo Cha udhibiti wa mitetemo na kelele ili kulinda afya ya binadamu bado haizingatiwi.

Waziri Jafo amedhihirisha hilo kwa kubainisha ongezeko la utoaji wa taarifa za malalamiko ya kelele hizo kuwa Katika kipindi Cha mwaka 2019/20 NEMC ilipokea jumla ya malalamiko 165 kutoka Mikoa ya Mbeya ,Dar Es Salaam,Dodoma,Arusha,Mwanza,Mororgoro na Tabora ambayo yalihusiana na kelele kutoka nyumba za ibada ,kumbi za starehe Pamoja na baa.

Licha ya hayo ameeleza kuwa Katika kipindi Cha Januari mpaka Machi mwaka 2021 ,NEMC walipokea malalamiko 93 kutoka Kanda mbalimbali ikiwemo Kanda ya kati (30),Kanda ya Kaskazini(12),Kanda ya ziwa(21),Kanda ya Nyanda za juu Kusini (6) na Kanda ya Mashariki (31).

"Katika kipindi Cha Januari hadi Aprili 2021 jumla ya malalamiko 20 yaliyoripotiwa Katika jiji la Dodoma pekee ambapo pia maeneo yaliyoongoza kwa kulalamikiwa ni maeneo ya nyumba za starehe na burudani Pamoja na nyumba za ibada,"amesistiza.

Licha ya hayo Waziri Jafo alieleza athari mbalimbali zitokanazo na kelele na mitetemo ambayo imezidi viwango Katika mitaa kuwa ni pamoja kupoteza usikivu,kuondosha utulivu,kupunguza ufanisi wa kazi,kuzuia watu wasipate usingizi,athari za kisaikolijiakwa watoto ,magonjwa ya moyo ,usumbufu kwa wagonjwa ,kupunguza umakini wakati wa kujisomea na kero kwa jamii.

"Kwa yeyote atakayesababisha kero zitokanazo na kelele na mitetemo kinyume na kanuni za usimamizi wa mazingira atakuwa amevunja sheria na adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni moja au kifungo Cha miezi sita jela ,"amesema na kuongeza;

"Adhabu hiyo itaendana na kufungiwa kwa biashara husika ,hata hivyo Ofisi yetu ya mazingira itaendelea kufanyia kazi kanuni za adhabu za makosa ya uchafuzi wa Mazingira ili kuongeza ukali wa adhabu za uchafuzi wa Mazingira nchini,"amesistiza Waziri Jafo.

 

 

Post a Comment

0 Comments