📌JOHN BANDA
KATIKA kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi wakulima wa
Mkoa wa Dodoma wameshauliwa kuendelea kulima mazao yanayostahimili ukame
ikiwemo zao la Mtama na Uwele.
Wito huo umetolewa jiji hapa na
Meneja Mradi wa Kilimo hifadhi kutoka Dayosisi ya Central Tanganyika DCT
Busela Yuga alipotembelewa kwenye Bada lao la Kilimo katika wiki ya Mazingira
inayoendelea viwanja vya JK.
Meneja huyo alisema kuwa,kama
iliyoelezwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kwamba ripoti ya tatu ya hali ya
Mazingira iliyofanya mwaka 2019 imeonyesha Mkoa wa Dodoma umeathiliwa kwa hekta
373,000 kwa shughuli za ukataji miti na misitu kwaajili ya matumizi ya Kuni na
mkaa.
" Kuathiriwa huko kwa kiasi
kikubwa katika Mkoa wa Dodoma kumepelekea Dodoma kuonekana kame na jangwa na
ndio Maana Sisi kama wataalamu wa Kilimo tunaendelea kuwaelimidha wananchi au
jamii kulima mazao yenyekustahimili ukame Ili wawe na Uhakika wachakula
nadani ya kaya," amesema Yuga.
Aidha amesema pia wameendelea kutoa
elimu ya upandaji kwa wakulima huku wakiwahamasisha wakulima kupanda mazao
yanayastahimili ukame ilikukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Tunawashauli wananchi wa mkoa wa
Dodoma kupanda mazao yanayostahimili ukame kama vile mtama na Uwele pia
wapande mazao jamii ya mikunde kama vile Mkunaa ,Canavalia,fiwi kwani mazao
hayo yamekuwa yanaifadhi maji na kurutubisha udogo,.
“Takwimu zinaonyesha endapo utafuata
utaratibu huo wa kupanda mimea jamii ya mikunde inamfanya Mkulima kulima mavuno
kwa wingi.
" Takwimu zinaonyesha mtu
akipanda mazao ya mikunde kwenye shamba lake alilolima uele na Mtama Mkulima
huyo anaweza kuvuna magunia Saba hadi 12 kwa shamba la kekta moja,"
alieleza Meneja huyo.
Hata hivyo amesema mradi huo wa
Kilimo hifadhi wenye lengo la kuwafanya wananchi na wakulima kuwa na uhakika wa
chakula ndani ya kaya ni mradi wa miaka mita na upo katika Wilaya tatu ambazo
ni Wilaya ya Dodoma mjini,Bahi na Chamwino.
Naye Yusuph Malenda mkulima wa
zao la Mtama katika kijiji cha Nghumbi amesema wamepatiwa elimu ya upandaji na
Mbegu bora kwa kuzingatia utaratibu maalumu.
Malenda amesema shamba
lake lina ukubwa wa hekari 2 ambapo anategemea kuvuna kilogram 200 za Mtama
ambapo ataweza kuwauzia wakulima wenzake 100 kwa shilingi 3000.
"Zao la Mtama ndio zao
mtambuka kwa kijiji cha Nghumbi kwani mimi ni mmoja wa wakulima wa mfano niliye
lima kwa Mbegu bora na manufaa yake ndio kama Haya yanayoonekana,”amesema Malenda.
0 Comments