📌DOTTO KWILASA
Hayo yameelezwa Jijini hapa na Balozi wa Nchi hiyo hapa nchini Lebius Tangeni Tobius alipotembelea ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kufanya nae mazungumzo ambapo Viongozi hao wawili wamekubaliana kushirikiana kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kwa umuhimu huo Serikali ya Namibia imesema kuwa itashirikiana na Serikali ya mkoa wa Dodoma kuimarisha maeneo ya Sekta ya Mifugo, Elimu na Sekta Binafsi ili kukuza masuala ya uwekezaji na biashara Mkoani hapa.
Balozi huyo amesema,kwa kutambua umuhimu wa kuwa Serikali hizo mbili zina historia ya pekee katika mikoa hiyo miwili ya Omusati na Dodoma ni vyema kwao kuendeleza mahusiano hayo ya kidiplomasia katika kukuza uchumi wa watu wake .
Amefafanua kuwa ,Mkoa wa Omusati una sifa na historia ya kipekee kwa kuwa ndio Mkoa ambao chama cha ukombozi wa Namibia cha SWAPO kilizaliwa huku Dodoma ikiwa ni Makao Maku ya Tanzania, makao makuu ya Chama Tawala cha CCM na Serikali ikiwa imehamishia shughuli zake hapa Dodoma.
Serikali ya Namibia itaendeleza na kuanzisha mahusiano ya kindugu kwa mikoa hii miwili kwa kutambua kuwa Mkoa wa Omusati una sifa na historia sawa kabisa na Dodoma ,undugu wetu ni hazina tunapaswa kuulinda.
Pamoja na Mambo
mengine amesema Katika makubaliano hayo watashirikiana kwenye eneo
la mifugo hususani uongezaji tija ya uzalishaji mifugo na kungeza thamani wa
mazao ya mifugo ikiwemo nyama, maziwa na ngozi
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kwa Kuwa kipaumbele chake ni kuinua kiwango Cha Elimu Mkoani hapa ataitumia fursa hiyo kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Namibia ambapo wataanzisha program za kubadilishana wanafunzi na wataalamu mbalimbali wa vyuo ili kubadilishana uzoefu na utaalamu.
Mbali na hayo
Mtaka ametumia fursa hiyo ya mazungumzo na Balozi Tobius kumualika
kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania vyenye sifa za kipekee
Duniani kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Taifa za Serengeti na Ruaha ili
kupitia yeye awaalike Watalii kutoka Namibia kuja Tanzania.
Licha ya hayo
viongozi wengi wa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika waliishi na
kupata mafuzo hapa nchini Tanzania.
0 Comments