📌JOHN BANDA
TANZANIA hupoteza zaidi ya Hekta 400,000 za Misitu kwa mwaka
kupitia shughuli mbalimbali za binadamu hali ambayo hupelekea mabadiliko ya
hali ya hewa ikiwemo ongezeko la joto.
Akizungumza jijini hapa ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya mazingira Meneja wa
Mawasiliano Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani(WWF) Joan Itanisa alisema
elimu inahitajika kwa wananchi ilikudhibiti uharibifu wa mazingira.
“Tunafanya kazi na serikali pamoja na wana jamii kuhakikisha
tunarejesha uoto wa asili ambao unaharibiwa na shughuli za binadamu ambapo
tumeamua kuanzisha kauli mbiu za
uhamasishaji ili kunusuru na kudhibiti hii hali ikiwemo kuanzisha
kampeni zinazolinda uoto wa asili,”alisema Joan.
Joani pia aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya
Rais Samia kwa kuendelea kusimamia Rasilimali za wanyamapoli kwa kuhakikisha
zinalindwa kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema kumekuwa na ongezeko la wanyamapoli wakiwemo
tembo,vifaru na simba hiyo inadhihirisha kuwa matukio ya ujangili yamepungua
kwa asilimia 100.
“Natoa pongezi kwa serikali na wadau wa wanyamapoli wakiwemo WWF kwa kuhakikisha wanapunguza ujangili ambao ilikuwa umeshamili lakini sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha idadi ya wanyapoli kama tembo na faru kuongezeka na kuongeza idadi ya watalii hivyo kuongeza pato la taifa,”alieleza
Kwa upande wake Afisa Ulaghabishi wa Sera za Mazingira WWF Nuhu Salala alitaja madhara yatojkanayo na uharibifu wa mazingira kwa binadamu.
Alisema kama hali ya uharibifu wa mazingira itabaki kama ilivyo sasa inaweza kupelekea ongezeko la joto na mabadiliko ya hali ya hewa na mmonyoko wa aridhi.
“Kama hatua stahiki zisipochukuliwa za haraka ikiwemo
kuanzisha kampeni za kupanda miti ilikurudisha uoto wa asili ulioharibiwa basi
tunaweza kushuhudia mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo jangwa, joto
kuongezeka, kubadilika kwa majira, na mafuriko,”alieleza
0 Comments