📌JOHN BANDA
WAZIRI wa mifugo na
uvuvi Mashimba Ndaki amewashauri wananchi kukubali kubadilika na kuingia kwenye
matumizi ya nishati mbadala ili kuweza kukabiliana mabadiliko ya tabia nchi
yanayosababishwa na uhalibifu wa mazingira
Pia amezitaka taasisi
mbalimbali zinazojihusisha na utengenezaji wa nishati hizo kuwarahisishia
wananchi upatikanaji wa uhakika pamoja na kuweka bei zafuu ambazo kila mtu
atazimudu bila kujali hali yake
Waziri amesema hayo
wakati alipotembelea maonyesho ya maadhimisho ya wiki ya mazingira
yanayofanyika jijini Dodoma ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
ni “tutumie nishati mbadala ili kuongoa mifumo ya Ikolojia” wakati
alipokuwa katika banda la Viridiam Tanzania LTD inayojihusisha na
utengenezaji wa mkaa mweupe unaotengenezwa kwa kutumia majani
Ndaki amesema wananchi
walizoea kulima, kufuga, kuvua bila tahadhari yoyote ya utunzaji wa mazingira
lakini sasa inabidi wakubali mabadiliko kwa kufanya shuhuli zao hizo za
kiuchumi kwa kutumia njia zinazoelekezwa na wataalamu
Alisema hata jikoni
wengi wamekuwa wakitumia mikaa na kuni hivyo ili kuweza kulinda na kutunza
mazingira ni vizuri watu wabadilike na kutumia nishati mbadala
Aidha alizitaka
taasisi zinazojishuhulisha na nishati mbadala kuwakikishia wananchi upatikanaji
wa uhakika pamoja na garama kuwa nafuu ili kurahisishia watanzania wote
Kwa mfano ninyi Viridiam Tanzania LTD hakikisheni mnakuwa na hifadhi ya kutosha mkaa huu mweupe ili kuwafanya watanzania waupate kiurahisi na bei iwe nafuu ili kila mtu aweze kuimudu.Kwa sasa mpo baadhi ya mikoa hakikisheni mnataka na kusambaa Tanzania nzima.
Mashimba Ndaki
Awali akitoa maelezo
mbele ya waziri mifugo na uvuvi na ujumbe wake meneja masoko wa
Viridiam Tanzania LTD inayojihusisha na utengenezaji wa mkaa mweupe Aristle
Nikitas alisema hivi sasa wanahifadhi ya zaidi ya tani laki nane za majani huku
wakiwa na heka 75 za kilimo hicho huko chunya wakati iringa ziki 100,000
Nae meneja mauzo Abuu
Habibu Ibrahimu amesema wanaziangatia ushauri wa serikali na kwamba wataufanyia
kazi kwa kuangalia jinsi ya kupunguza bei toka bei ya sasa ya mkaa mweupe
unaouzwa 2000 kwa kilo 2 na kuushusha zaidi
Aidha alisema kwa sasa
wamejikita katika mikoa ya mbeya, Pwani, iringa, mwanza, na Dodoma ambapo kwa
sasa wanaendelea kutoa elimu kisiwani Mafya na kwamba lengo lao ni kusambaza
huduma hiyo nchi nzima
0 Comments