📌MWANDISHI WETU
SERIKALI imeahidi
kuheshimu na kuzingatia mifumo ya
kulinda haki za binadamu kwa mtu
mmoja mmoja,makundi na Jamii kwa ujumla.
Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Waziri wa Katiba na
Sheria Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa kikao baina ya Wizara ya Katiba na
Sheria na Mtandao wa watetezi wa Haki za
Binadamu.
Prof Kabudi amesema kuwa
hiyo ni pamoja na kubuni na kutekeleza mikakati ya kukuza,kulinda na
kutekeleza misingi ya haki za binadamu na wajibu wao.
Kama Serikali tuna jukumu pia la kuweka mazingira rafikio kwa wananchi kufikia vyombo vinavyo simamia haki katika ngazi zote,kulinda haki za Kikatiba za Wananchi wanaoshiriki katika mijadala mbalimbali inayohusus maendeleo ya Taifa lao na kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Katiba na sheria ili kuimarisha misingi ya kikatiba,demokrasia,utawala bora na utawala wa sheria.
Aidha alifafanua Serikali imekuwa inachukua hatua ya kupunguza mrundikano wa
kesi Mahakamani ikiwa ni pamoja na kuimarisha
mfumo wa Wasajili wasaidizi katika Halmashauri zote ili kuwezesha
uratibu na utoaji msaada wa kisheria katika masuala ya mirathi na ndoa.
“Hii ni katika kiuhakikisha huduma bora za Sheria
zinapatikana kwa wakati na gharama nafuu
kwa kuongeza wataalam,miundombinu,vitendea kazi na kusogeza huduma karibu na
wananchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha Vyombo vya Sheria kwa kuongeza wigo wa
huduma za utoaji wa haki nchini””,Alisistiza Profesa Kabudi.
Hata hivyo amesema Serikali
ipo tayari kushirikiana na Watetezi wa
Haki za Binadamu pamoja na Wadau
wengine wote wasio wa Serikali ambao wapo tayari kuunga mkono jitihada za
Serikali za kukuza na kulinda Haki za Binadamu
na Watu.
Waziri Kabudi pia amesema Wizara yake itaendelea
kushirikiana na wadau wa kutetea Haki za binadamu ili kuhakikisha wananchi
wanapata haki kama ilivyo ainishwa
katika katiba na ilani ya Chama cha Mapindizi (CCM) 2020/2025.
Tuko tayari kushirikiana na wadau ninyi muhimu kwenye masuala ya kupigania haki za wananchi tunajua kuwa mtakua na vipaumbele vyenu muhimu na serikali pia itakuwa na vipengele vyake ambavyo vinalenga kukuza haki za binadamu na kuleta maendeleo katika nchi yetu
Kwa Upande wake Mratibu wa Mtandao wa Onesmo Olengurumwa THRDC alisema serikali inatambua kuwa mfumo bora wa sheria ndio msingi wa kutekeleza matakwa ya katiba,Sera,na mpango wa nchi.
Alisema asasi za kutetea haki za binadamu zimekuwa na
mchango mkubwa kwa jamiii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki
zao kwa wakati.
Asasi za kiraia zimekuwa zikifanya vizuri sana hapa nchini tunaomba serikali itambue mchango wa asasi hizo na kuongeza ushirikiano ili ziendelee kufanya vizuri kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla
Olengurumwa aliihakikishia serikali kuwa mashirika ya
kutetea haki za binadamu yataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha
wananchi wanapata haki zao kwa wakati bila vipingamizi vyovyote.
0 Comments