MATUMIZI YA DIZELI KWENYE MIRADI YA MAJI YAUMIZA KICHWA RUWASA

 


📌RHODA SIMBA

KATIKA harakati za kuacha matumizi ya mafuta ya dizeli katika miradi ya maji Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imesema  itabadilisha mifumo hiyo na kutumia nishati mbadala ya umeme wa gridi na sola.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mhandisi Mkuu wa RUWASA Dodoma,Fredrick Mageni alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya wiki ya mazingira ambapo amesema ili kuweza kutunza mazingira wataacha matumizi ya genereta ambazo zinatumia dizeli ambazo zinatota moshi nakusababisha uchafuzi wa mazingira.

Amesema kwa baadhi ya maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya umeme wa gridi injini za pampu za maji zilitumia mafuta ya dizeli kuendeshea mitambo jambo ambalo halina manufaa kwa sasa.

Amefafanua kuwa,Tanzania ikiwa Katika harakati za kuenzi na kutunza mazingira kila Taasisi kwa namna yake zinapaswa kubuni mbinu za uhifadhi na kuwezesha jamii kuzoea Hali hiyo.

Tunaelekeza nguvu katika nishati mbadala,Katika huduma zetu tutahakikisha tunaondoka na matumizi ya dizeli na kutumia umeme wa Sola,hali hii itaongeza nguvu katika uhifadhi wa mazingira

Pamoja na hayo katika kutekeleza kwa vitendo na kuhakikisha wananchi vijijini  wanapata huduma ya maji safi na kwa wakati Mhandisi huyo pia alieleza mikakati ya kuanzisha huduma ya mita za malipo ya kabla kwa Vijiji 77 vya mkoa wa Dodoma ambazo zinatumia umeme jua.

Aidha ametaja Kijiji Cha Zanka kilichopo Wilaya Bahi tayari kimeshaanza kutumia huduma hiyo  na pampu zinazotumika ambazo  ni salama na rafiki kwa mazingira.

"Tumegawa kadi ambazo zimetengenezwa kwa Mfumo wa malipo ya kabla kwa kila mkuu wa kaya kikiwezesha kupata huduma hiyo,hii inamaanisha kwamba bila kadi hiyo huwezi kupata maji,"alisema na kuongeza;

Mteja wa Maji atatakiwa kuweka fedha kwa mfumo wa vocha Katika kadi hiyo kwa kutumia namba ambayo ipo juu ya kadi ili kuwezesha kupata huduma.

Hata hivyo Mhandisi huyo wa RUWASA amebainisha faida za matumizi ya mita za malipo ya kabla kuwa ni Pamoja na mtumiaji kuwa na uhakika wa kupata huduma ya maji wakati wote na mtumiaji kulipia gharama kulingana na maji aliyotumia.

Faida nyingine ni kupunguza matumizi ya maji yasiyo ya lazima ambapo kabla ya huduma hiyo hakukuwa na utaratibu mzuri wa matumizi ya maji ambapo watu walitumia maji mengi kuoshea ndoo za maji bila kujali upotevu wa maji hali iliyopelekea maji mengi kupotea.

Kupitia mita hizi ,hakuna tena masuala ya wizi wa maji,kila mtu atapata maji na kulipia ,hali hii itaiongezea Serikali mapato ya hakika bila udanganyifu wowote.

Post a Comment

0 Comments