KILANGI AWATAKA MAWAKILI WA SERIKALI KUJIELIMISHA



📌DOTTO KWILASA

MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi,amewataka Mawakili wa Serikali Nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria Ulimwenguni kulingana na umuhimu wa  kazi yao wanayoifanya ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Profesa Kilangi ametoa wito huo  Jijini hapa wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa Serikali yenye lengo  la kuwaongezea uwezo katika stadi za uendeshaji madai ya usuluhishi kwa kuwapa ujuzi ambayo yameandaliwa na  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Amebainisha kuwa  mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuwanoa Mawakili hao ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya Sheria ambayo yamekuwa yanatokea kila siku ulimwenguni.

Niishukuru sana ofisi ya Wakili mkuu wa Serikali kwakuandaa mafunzo haya ambayo ni muhimu na yatawapa uwezo na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa mawakili kwa lengo la maslahi ya umma

 Hayo yote ni maeneo muhimu sana sababu ya mabadiliko katika majukumu yenu na wengi wenu mtashirikiana na wakili mkuu wa serikali kwaajili ya kusimamaia kesi hasa za serikali ndani na nje ya nchi hivyo ni lazima muwe na ujuzi wa kuweza kusimamaia mashauri hayo,”Alisistiza.

Aidha alifafanua kuwa Mwaka 2019 walilazimika kuendesha kesi mbele ya mahakama kuu ya biashara London uingereza ndani ya mwezi mzima hivyo ni lazima waweze kuendesha hizi kesi ndani nan je ya nchi kutokana na wigo kuongezeka.

Sambamba na hilo amesema Mafunzo hayo yataongeza uwezo na weledi katika suala zima la usuluhishi la madai mbalimbali hivyo muendelee kujielimisha.

Kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoikabili ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ikiwemo uhaba wa mawakili wa Serikali amesema ni muhimu kwa Taaisi zote za Serikali wakashirikiana ili kukabiliana na changamoto hizo.

 Katika hatua nyingine amesema bado mpango wakuanzisha chuo cha wanasheria wa serikali upo ambao kuanza kwa chuo hicho utasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mawakili wa Serikali.

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata amesema ofisi hiyo ilipewa jukumu lakuendesha madai ya kesi ndani nan je ya nchi na kupitia mafunzo hayo yanaenda kuwaweka katika mtazamo mmoja wa uendeshaji wa mashauri kwaniaba ya Serikali na Taasisi zake huku akibainisha mafanikio na changamoto mbalimbali.

Kuhusu mafanikia amesema katika Kipindi cha Mwaka 2019/2020, Ofisi ya Wakili mkuu wa Serikali ilifanikiwa  iliokoa fedha zinazotokana na mashauri yaliyofunguliwa dhidi ya Serikali na Taasisi zake trilioni 11.4ambazo zingelipwa kwa watu wasiostahili na kuisababishia serikali hasara pia ofisi iliendesha mashauri mbalimbali na kurejesha mali zilizochukuliwa na watu wasiostahili jumla ya amshamba 106 ya serikali yalikuwa mikononi mwa watu asiostahili.

Pia akaeleza changamoto zinazowakabili ni uhaba wa mawakili ambapo walipo ni 188 mahitaji ni zaidi ya mawakili 308 pamoja na uhaba wa usafiri.

 

Post a Comment

0 Comments