📌DOTTO KWILASA
ASKOFU mkuu na
Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kusini Mwa Tanzania Mch.
Mark Walwa Malekana ametoa wito kwa vijana kuwa na mpango
mkakati wa kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana ya
utegemezi kutoka kwa wazazi.
Mchungaji
Malekana amebainisha hayo jana jijini hapa katika mwendelezo wa mkutano
wa shangwe katika njia Yake ambapo alisema kumekuwepo na kasumba kwa
baadhi ya vijana kuwa na uvivu na kutegemea kwa wazazi ambao ni wazee
hivyo ni wakati sasa umefika kwa vijana kufanya kazi kwa bidii.
Aidha,Mchungaji
Malekana ametoa hamasa kwa kwa vijana na watanzania kwa ujumla kuacha
anasa na kujikita zaidi kufanya mambo yampendezayo Mungu.
“Vijana unakuta
wapo kwenye vilabu vya pombe wanafanya vitu wa anasa na wanafanya dhambi za
kila aina kwenye baa wananunuliana bia hawajitabui hivyo natoa wito
wajinyenyekeze kwa Mungu’’amesema.
Sanjari na hayo
Mchungaji Malekana ametoa onyo kwa baadhi ya washiriki wanafiki
wanaotenda matendo maovu kwa kujificha ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo zisizo za
maadili pamoja na kuvunja shule Sabato ingawa wakiujua ukweli na kusisitiza
kutii amri za Mungu.
’’Nawaambia
wana wa Afrika fanyeni kazi kwa siku sita na kuendelea kutii amri za
Mungu na kuvaa mavazi yaliyo na maadili nay a kumpendeza Mungu’’amesema.
Kuhusu suala la
uimbaji kanisani,Mchungaji Malekana alitoa wito kwa kwaya zilizo ndani ya
kanisa la Waadventista Wasabato kkuimba kwa kufuata kanuni za uimbaji
ndani ya kanisa huku akitumia fursa hiyo kuipongeza kwaya ya
Jangwani kutoka Mkoani Shinyanga kwa kuelendelea kuimba kwa utulivu bila papara.
Katika hatua
nyingine Mchungaji Malekana aliwaasa vijana waliopotea kwa kujikita katika dawa
za kulevya,uasherati kuona haja ya kurejea kwenye usafi wa moyo.
0 Comments