📌MWANDISHI WETU
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na usalama imeridhishwa na maendeleo yanayofanywa
na Jeshi la Magereza ikiwa ni utekelezwaji wa maono ya aliyekuwa rais wa awamu
ya sita hayati Dkt.John Magufuli,aliyelitaka jeshi hilo kujitegemea.
Akizungumza baada ya ziara fupi ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na jeshi hilo katika makao makuu
yake katika eneo la Msalato jijini Dodoma,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mussa Azan
Zungu alisema hatua iliyofikiwa na jeshi hilo ni ya kupongezwa.
Katika ziara hiyo Kamati ilitembelea kiwanda cha
samani ambacho hadi ukamilikaji wake kimegharimu takribani shilinig bilioni 2,
nyumba za askari 150 wa jeshi hilo pamoja na majengo ya Makao Makuu.
Ni kazi nzuri imefanywa na Meja Jenerali wa Magereza Suleimani Mzee,tulipokuja hapa (Msalato) mwaka jana tulipouona msingi wa jingo la kiwanda cha samani hatuona matumaini ya kukakimilika kwake,lakini tunarudi baada ya mwaka kimekamilika.
Zungu.
Kamati hiyo ilibainishwa kwamba licha ya serikali kupunguza kupeleka fedha kwa ajili ya chakula katika jeshi la Magereza lakini jeshi hilo halijateteleka hivyo hiyo ni ishara tosha kwamba katika miaka michache ijayo linaweza kujiendesha lenyewe bila kutegemea ruzuku ya chakula kutoka serikalini.
Zungu pia amesema katika maagizo 6 waliyotoa katika
ziara ya mwaka jana,Uongozi wa jeshi hilo umeyatamiza kwa ufanisi ikiwemo ujenzi hospitali na karakana ya utengenezaji wa magari ili
kupunguza mzigo kwa serikali.
“Tuliwaagiza pia waanzishe karakana na leo tumeiona
imekamilika.Hii itaisaidia kupunguza mzigo wa matengenezo ya magari ambayo huwa
yanapelekwa kwenye karakana binafsi kwa ajili ya matengenezo.” Alibainisha
Zungu.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini
Kamishna Jenerali wa Magereza Meja Jenerali Suleimani Mzee alisema hatua ya
jeshi hilo kujitegemea imepunguza madeni kutoka kwa wazabuni waliokuwa
wanatumika kulisha wafungwa na askari wa jeshi hilo.
Kamishna Jenerali Mzee alibainisha kuwa kabla ya
kujitegemea serikali ilikuwa inatoa kiasi cha takribani milioni 800 hadi 900
kwa ajili ya chakula tangu waanze kujitegemea mwezi Machi mwaka 2020. Pia
amewahakikisha Kamati hiyo kwamba samani zitakozalishwa katika kiwanda hicho
zitakuwa zenye ubora na bei itakuwa nafuu ili kila Mtanzania aweze kumudu hali
itakayoiongezea kipato cha uhakika jeshi hilo.
0 Comments