📌DOTTO KWILASA
IKIWA ni wiki ya Utumishi wa Umma,Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetoa msaada wa mashuka 431 kwenye vituo vinne vya kutolea huduma za afya vya jiji la Dodoma ili kuboreshà huduma kwa jamii.
Hayo yamesemwa Jijini hapa
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari .
Chibulunje amesema, mashuka
hayo yatakwenda kwenye vituo vya afya vya Makole,Hombolo ,Mkonze na Kikombo
jijini hapa.
Hii ni wiki ya Utumishi wa Umma na leo ndio Kilele cha maadhimisho yake,hivyo EWURA tunaadhimisha siku hii kwa kutoa msaada kwenye vituo vya afya vya jiji la Dodoma kama mchango wetu katika kuboresha huduma za afya.
Chibulunje
Naye Mganga Mkuu wa
Jiji la Dodoma Dkt.Endrew Method akizungumza mara baada ya kupokea msaada
huo wa mashuka amewashukuru Ewura na kuwaomba kuendelea kujitoa kusaidia katika
maeneo mbali mbali ya afya.
Amesema kuwa hiyo siyo mara
ya kwanza kwa EWURA kuwasaidia moja kwa moja jamii ,kwani kuna
wakati pia waliwasaidia fedha ambazo zilielekezwa kwenye huduma ya mama
na mtoto na kuongeza kuwa mashuka hayo yanakwenda kuchochea utoaji wa
huduma bora kwa jamii.
Katika kituo cha afya Makole ,takribani wakina mama 120 wanajifungua kila wiki ,hivyo tunapoboresha huduma tunalenga kuisaidia jamii .Dk.Method
Dkt.Method pia ametumia fursa
hiyo kuwatahadharisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa wa
corona.
"Nitoe wito kwa jamii
kujihadhari na Corona kwa kuepuka mikusanyiko,kuvaa barakoa na kutumia
vitakasa mikono,"amesema.
0 Comments