📌DOTO KWILASA
CHAMA cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) kimeilalamikia Idara ya Elimu
nchini kwa kushindwa kuwa na mtaala maalumu wa kufundishia wanafunzi viziwi
mashuleni na kusababisha kushindwa kuendelea na Elimu ya juuu.
Hayo yamesemwa leo hii Jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji CHAVITA
Dickson Mveyange wakati akizungumza kwenye mafunzo na kampeni kuhusu ukiziwi na
lugha ya alama yaliyohusisha wadau wa Elimu,wazazi wa watoto wenye ukiziwi na
wadau wa maendeleo.
Amesema,mitaala inayotumika mashuleni ni ya jumla na
haiwazingatii viziwi Pamoja na kuwa kina tofauti ya wanaosikia na viziwi
hali ambayo ni kikwazo kwa watoto hao ambao wanatakiwa kupewa Elimu maalum
badala ya Elimu ya jumla.
Licha ya hayo Mkurugenzi huyo amesema,licha ya Idara ya
maendeleo ya Jamii kuridhia kuwepo kwa lugha ya alama lakini inaonekana Jambo
hilo bado halijatekelezwa ipasavyo na kusababisha wanafunzi wengi viziwi
kushindwa kuendelea na masomo Kutokana na ugumu wa lugha ya Mawasiliano.
Bado Kuna mapungufu mengi,tunahitaji maboresho zaidi ili kuweka usawa kwa jamii na viziwi nao waweze kusoma bila kubaguliwa,bado ukosefu wa misamiati ya masomo ya sayansi, uraia na historia bado ni changamoto,vitu vyote hivi vinapaswa kuangaliwa upya
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Mtaala uliopo unawanyima
wanafunzi fursa ya kufikia malengo yao katika masomo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Nidrosy Mlawa aliitaka
jamii kuwashirikisha viziwi kwa mambo yote ili maendeleo yasimwache mtu.
Amesema,ili kuifikia Tanzania ya ndoto za walio wengi lazima
kuwepo marekebisho Katika mitaala ya Elimu ili watu wenye mahitaji maalumu
wasibaki nyuma.
Kuna hili suala la ufinyu wa muda katika vipindi, sehemu kubwa ya wanafunzi wenye uziwi hawawezi kumaliza maswali katika majaribio ya saa moja na nusu kwa sababu ni ngumu sana kwao kusoma sentensi ndefu na hata kwenye hesabu swali moja la kufanya dakika mbili wao hutumia dakika tano ili waweze kupata jibu sahihi.
Amesema,Mtaala wa elimu ni mwongozo wa masomo unaotoa dira ya mafunzo
yanayotakiwa katika utoaji wa mafunzo kwa wanafunzi katika ngazi fulani ya
elimu
Kutokana na hayo Baadhi ya walimu wanaowafundisha wanafunzi
wenye uziwi walitumia nafasi hiyo pia kueleza changamoto wanazokutana nazo
wanafunzi hao wawapo shuleni huku wakiiomba Serikali kulivalia njuga suala hilo
ili kuweka usawa.
Mwalimu Marry Masangula kutoka shule ya msingi
Kigwe-Viziwi Dodoma,ameeleza kuwa wa sasa wanafunzi wenye uziwi hutumia
mda mwingi hadi kumaliza elimu yao ya msingi kutokana na kutokuwepo kwa
miundombinu sahihi kuwawezesha kuelewa masomo.
Amesema, ili kumaliza elimu yao ya shule ya msingi kunakuwa na
vikwazo vingi Sana ukikinganisha na wanafunzi wasio walemavu ambao
hutumia miaka saba tu kumaliza elimu hiyo.
"Ili waelewe vyema wanafunzi wenye uziwi kama sisi walimu
tunapaswa kutumia zaidi lugha ya alama pamoja na vitendo kuwaelimisha lakini
Jambo hili bado ni gumu kwa kuwa walimu pia hawatoshelezi,"anasema
Amesema,Kwa kawaida ratiba iliyopo kwenye mtaala wa sasa inampa
mwalimu dakika 40 tu za kufundisha ikiwa ni muda sawa kwa wanafunzi wote wa
shule ya msingi wenye mahitaji maalum na wasio walemavu,Dakika
ambazo zaelezwa kutotosha kuwafundisha watoto hao wenye mahitaji
maalum.
0 Comments