📌NTEGHENJWA HOSSEAH-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu(Mb) amesema mtumishi wa Tawala za Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa atakayeharibu katika kituo chake cha kazi
hataruhusu ahame isipokua atamuwajibisha akiwa katika kituo chake cha kazi.
Waziri Ummy ameyasema hayo katika ziara yake
Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na
Kamati ya Fedha pamoja na Menejimenti ya
Halmashauri hiyo tarehe 04.05.2021.
Sitaruhusu mtumishi aharibu Chemba kisha ahamishiwe Kongwa, niwahakikishie kuwa ntamshughulikia akiwa hapa hapa Chemba na nikibaini ana hatia ntamchukulia hatua stahiki
Mhe. Ummy.
Aliongeza kuwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa walizoea kufanya ubadhirifu wa miradi ya maendeleo haswa ya Elimu, Afya na Barabara na wakishaona mradi haujakamilika au unatuhuma hizi na zile anahama sio wakati wa Uongozi wangu hakuna atakayehama kukwepa tuhuma.
Na hapa Chemba wote waliohama sababu ya kutokukamilisha miradi ya maendeleo kama Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya watarudi kuja kujibu tuhuma zao
Mhe. Ummy.
Waziri Ummy yupo katika ziara za kukagua miradi ya
maendeleo na kuzungumza na kamati za
Fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Bahi na kongwa.
0 Comments