WAZIRI NDAKI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI SEKTA YA UVUVI,ASISITIZA NIDHAMU KWA WATUMISHI

 



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki,akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Uvuvi kilichofanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.

📌ALEX SONNA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi,Mhe.Mashimba Ndaki amelitaka  Baraza la Wafanyakazi sekta ya uvuvi kusimamia ushirikishwaji wa  watumishi katika utendaji kazi wa kila siku ili kuondoa manung’uniko.Pia amesisitiza umuhimu wa kusimamia uadilifu,uaminifu na nidhamu kwa watumishi wa umma.

Hayo ameyasema leo Mei 10,202,Jijini Dodoma  wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi sekta ya uvuvi  amesisiitiza juu ya umuhimu wa watumishi kushirikishwa katika utendaji kazi wa kila siku ambapo amedai kwa kufanya hivyo manung’uniko yatapungua.

Mhe.Ndaki amesema kuwa lazima kuwepo  umuhimu wa ushirikishwaji wa watumishi katika ufanyaji kazi katika vitengo vyote,sisi wote tunajua ushirikishwaji ni jambo la msingi mahali pa kazi,hasa kwenye mambo yanayohusiana na hizo idara na taasisi na vitengo vyetu tukiwashirikisha wafanyakazi tutapunguza manung’uniko.

Hata hivyo amesema kuwa anaelewa  umuhimu wa jambo hili lakini pia,sheria inatutaka tufanye hivyo. Rai yangu kwenu juu ya jambo hili tuendelee kushirikishana kwenye mambo muhimu na yanayotuhusu kama wafanyakazi kabla ya kufikia uamuzi ili tufikie uamuzi kwa pamoja

Tukifanya hivyo itasaidia sana kwenye mambo mengi yanayohusu masilahi yetu na ustawi wetu mahali pa kazi na yanayohusu mipango yetu itasaidia sana kwenda pamoja na kuwa a mwelekeo mmoja na kwenda kwa umoja.

Waziri Ndaki

Pia,amewataka viongozi wa baraza hilo kusimamia nidhamu pamoja na kuchukua hatua pindi yanapotokea mambo ya ukosefu wa nidhamu mahala pa kazi.

“Viongozi kwenye ngazi zote tunatakiwa kusimamia na kuchukua hatua,inapotokea mambo ya kinidhamu ya watumishi na watendaji wanapokuwa  yameenda sivyo lazima viongozi wa  ngazi ya idara, taasisi,kitengo,wizara lazima tusimamie ipasavyo kwa sababu kutofanya hivyo ni kinyume cha mkataba wa huduma kwa wateja pamoja na  mkataba mwingine  wa huduma bora kwa wafanyakazi.


Baadhi ya wajumbe wakifatilia hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Uvuvi 


Pia,aliwataka kusimamia mkataba wa huduma bora kwa wafanyakazi ambao una mambo ya msingi kama kutochelewa kazini,kukosa uadilifu na mambo ya kutoa na kupokea rushwa kwani hayo ni masuala ya msingi.

“Niwaombe sana ndugu wajumbe masuala ya uadilifu,uaminifu,nidhamu kazini ni masuala ya msingi sana uzuri ni kwamba kuna sheria na taratibu na kanuni zinazotuongoza katika mambo haya, kwahiyo tunapaswa kuziangalia na kuziheshimu ili kwamba tuweze kutoa huduma kwa wananchi wakati kwa kadri tunavyotegemewa.

Mimi pia kama Waziri ambaye nasimamia shughuli za uendeshaji na utendaji kazi wa  kila siku wa Wizara haitoshi tu kwamba mimi sihusiki na masuala ya kinidhamu ya kimaadili na uadilifu lakini natakiwa kuhakikisha kwamba Wizara kwa ujumla inaendana na masuala ya nidhamu kazini inaendana na masuala ya uadilifu na uaminifu kazini.

Pia,amewataka wafanyakazi hao kujadili kwa ukamilifu bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi  kwa mwaka wa fedha 2020-2021 na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha sekta ya uvuvi 2021-2022.

“Mtapitia taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020-2021 na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha sekta ya uvuvi 2021-2022,nitumie fursa hii kuwaomba kujadili kwa ukamilifu taarifa zote hizo mbili kwa uwazi kwa kina kisha mtoe maoni yenu,”amesema.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Uvuvi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah,akitoa maelezo ya awali ya kikao hicho kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mhe.Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki


Awali,Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah, amesema  kikao hicho kitakuwa na agenda za  wajibu wa mwajiri,Tughe na wajumbe wa baraza mahala pa kazi pamoja na  agenda kuhusu taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2020- 2021 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2021-2022.


“Kikao cha leo ni cha kwanza  kutokana na kwamba sekta ya uvivi ni kama ilikuwa imeanzishwa upya kwa kuwa kulikuwa kuna upungufu mkubwa wa watumishi hivyo katika kipindi cha mwaka 2018- 2020 kulikuwa kuna jitihada mbalimbali za kukamisha taratibu za kuwa na baraza  ikiwemo kuandaa mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi na kutiwa saini na Tughe,”amesema Dkt.Tamatamah

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki,akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kufungua  kikao cha Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Uvuvi kilichofanyika leo Mei 10,2021 jijini Dodoma.



 

Post a Comment

0 Comments